PENNY:DIAMOND ANAWEZA KUFANYA SHOO KATIKA HARUSI YANGU

Mtangazaji  wa 93.7  E-FM  kupitia  kipindi  cha  Genge,  DVJ Penny  ambaye  wiki  kadhaa  zilizopita  picha  zake  zilisambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  akiwa  amevishwa  pete   ya  uchumba  huku  mwanaume  aliyefanya  tukio  hilo  akiwa  ni  kitendawili, hatimaye  mwanadada  huyo  ameibuka  na  kumuweka  wazi  mpenzi  wake…..

Akiongea  na  mwandishi  wetu, rafiki  wa  karibu  wa  Penny  amesema  kuwa  jamaa  aliyemvalisha  pete  ni  kigogo  mwenye  pesa  chafu  anayemiliki  migodi  kadhaa  ya  madini  anayefahamika  kwa  Jina  la  Johnson  raia  wa  Angola….

Akiongea  kwa  kirefu  zaidi, msichana  huyo  alisema,” Watu  wanaumiza  vichwa  vyao  kufikiri  ni  nani  aliyechukua  maamuzi  magumu  ya  kumvisha  pete  Penniel, lakini  ukweli  ni  kwamba  huyo  jamaa  ni  mtu  mwenye  pesa  chafu  raia  wa  Angola,”
PENNY 
Rafiki  huyo  amesema  kuwa  kutokana  na  jeuri  ya  pesa  ya  kigogo  huyo, Penny  anatarajia  kufanyiwa  bonge  la  harusi  na  watafanya  kila  namna  ili  Diamond  awe  mtumbuizaji  katika  sherehe  hiyo….

“Huko  kwao  Johnson  anamiliki  migodi  zaidi  ya  kumi  ya  Almasi  na  yupo  hapa  nchini  kwa  ajili  ya  uwekezaji, anampenda  sana  Penny  na  ameahidi  kumfanyia  kila  atakacho,”  alisema  msichana  huyo.

Baada  ya  kupata  umbea  huo,  Mwandishi  alimtafuta  Penny  kupitia  simu  yake  ya  mkononi  na  kumhoji  juu  ya  taarifa  hizo  ambapo  alikiri  kuwa  na  mchumba  na  kusema  ndoa  iko  karibuni.
penny
“Nimeshakuwa  sasa, hivyo  nahitaji  kuolewa,  ni  kweli  nina  mchumba  na  ni  raia  wa  Angola, Inshaaalah  Mungu  akipenda  mambo  mazuri  yanakuja, ntakutaarifu,” alisema  Penny
Alipoulizwa  kuhusu  Diamond  kutumbuiza  kwenye  harusi  yake, Penny  alijibu;
“Kutakuwa  na  wasanii  wengu  tu  sasa  na  yeye  kama  atapokea  mwaliko  wa  kuja  kutubuiza  atapatiwa  nafasi, akiona  vipi, halazimishwi.”

Comments