OMMY AZIDI KUWACHANGANYA VANESSA MDEE NA JOKATE

Habari ya mjini katika ulimwengu wa mastaa wa Kibongo ni madai ya Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ kuwachanganya kimalovee, mastaa wenzake, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’ na Vanessa Mdee ‘Van V’ au V-Money, Ijumaa Wikienda limeinyaka.  
 
 Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akipozi kimahaba na Vanessa Mdee, ‘V-Money’.  

Kikizungumza na gazeti hili namba moja kwa habari za mastaa Bongo, chanzo makini kilisema Jokate na Vanesa kwa sasa ni kama chui na paka kufuatia hivi karibuni Jokate kudaiwa kuingilia penzi la mwanzake na mpaka sasa eti ndiye aliyeshikilia usukani.
“Sasa hivi Jokate na Ommy ni mahaba niue kwani mara nyingi wanakuwa pamoja.
“Hadi Jokate anakwenda geto kwa Ommy jambo ambalo limesababisha yeye na V-Money kutoelewana kwani awali ndiye alikuwa kiburudisho cha Ommy,” kilidai chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizi, mwanahabari wetu alimtafuta mhusika mkuu Ommy Dimpoz ambaye alikuwa na haya ya kusema: 
 
Mbongo-Fleva, Omary Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ akishow love na Jokate Mwengelo ‘Kidoti’. 

“Ehee! Ndiyo nasikia kwako, kwani wasanii haturuhusiwi kupendana jamani, hata Mwalimu Nyerere (Baba wa Taifa) alisema tuwe pamoja kwa hiyo Jokate ni rafiki yangu wa karibu na huyo Vanessa sijawahi kuwa na uhusiano naye but (lakini) alikuwa mshikaji tu.”
Juhudi za kuwapata Jokate na Vanessa ziligonga mwamba baada ya simu zao kuita bila kupokelewa hivyo jitihada zinaendelea ili kila mmoja aeleze la moyoni mwake.Juzikati picha za Jokate na Ommy wakiwa kimahaba zilizagaa kwenye mitandao mbalimbali hali iliyozua viulizo kibao kwa mashabiki wao.


Comments