Shabiki maarufu wa Michael Jackson ambaye alikuwa ni Mfalme wa Musiki wa Pop ambaye kwa sasa ni marehemu, ametumia zaidi ya pauni za Uingereza 2000 (sawana shilingi za Tanzania 5,590,621) kuchubua ngozi yake ili kufanana na mwanamuziki huyo.
Shabiki huyo Mbrazil, Antonia Gleidson Rodrigues, 32 ambaye amejitangaza kuwa mtu pekee anayefanana na Michael Jackson kuliko wote nchini Brazil, amefanyiwa upasuaji ili kufanana na Michael huku akitumia zaidi ya saa 4 kila siku kujifunza kucheza filamu na muziki kama Michael Jackson.
“Gleidson Jackson”, kama ambavyo hupenda kuitwa, alifanyiwa upasuaji mara ya kwanza miaka mitano iliyopita, ambapo alirekebishwa pua ili aweze kuimba sauti ya juu.
Baada ya upasuaji wa kwanza, mkazi huyo wa Fortalenza, Brazil aliendelea na mkakati wake wa kufanana na mwanamuziki huyo wa pop kwa kudungwa tindikali ili kuufanya uso wake kuwa mweupe, pamoja na sindano zilizofanya maeneo yanayo zunguka macho kubadilika.
Gliedson ambaye alikuwa mwalimu wa maigizo, alifanyiwa upasuajia ili kuziba nafasi zilizopo meno yake, kurekebisha kope kwa kuzichora kama tattoo. Sasa hivi shabiki huyo anakusanya pesa kwa kumuigiza Michael Jackson ili aweze kulipia upasuaji mwingine zaidi.
Anasema: “Kama nitamudu gharama, nafikiria kufanyia kazi magego iliniondokane na mikunjo ya mdomoni – nataka pia kuchonga nyusi. Ningependa pia paji langu la uso lichorwe (tattoo) na kuchonga pua yangu iwe nyembamba zaidi.”
Gleidson alivutiwa kuwa kama Michael Jackson alipokuwa na miaka 19 baada ya mwanafunzi mwenzake kumwambia anafanana na mkongwe WackoJacko. “Ilikuwa ngumu, nilitaniwa kwa siku 15. Mwishowe nikanasa – nikaambukizwa.”
Comments
Post a Comment