Rubani wa kwanza wa kike nchini Kenya sasa amepata mafanikio zaidi kwa kufuzu kuwa rubani wa kwanza mwanamke barani Afrika kushika usukani wa ndege za kisasa aina ya Boeing 787 Dreamliner.
Imemchukuwa Rubani Irene Koki Mutungi kipindi cha zaidi ya miaka ishirini kufanikiwa kuvunja pingamizi zote zinazowazuia wanawake kuingia katika taaluma hiyo inayotawaliwa na wanaume.
kwa kipindi kirefu-Rubani huyo ambaye sasa amepewa jina la Boeing Girl anasema mambo bado.
Mwandishi wa BBC Denis Okari alifanikiwa kukutana naye baada ya kutua kutoka ndege hiyo ambayo ni ya nne katika msafara wa ndege mpya aina ya Dreamliner zinazomilikiwa na shirika la ndege la Kenya Airways.
Hamu ya kuwa rubani kwa Koki ilitokana na kazi ya babake ambaye pia alikuwa rubani
Koki alikuwa mwanamke wa kwanza rubani kufanya kazi katika shirika la ndege la Kenya kwa miaka sita.
Alianza kazi yake ya kuendesha ndege mwaka 1993.
Kazi yake ya kwanza hata hivyo ilikuwa aliposhika usakani wa ndege ya Fokker 50 kwenda Kisumu Magharibi mwa Kenya kama kazi ya kwanza ya kulipwa.
Alianza kupenda kuendesha ndege alipokuwa msichana mwenye umri wa miaka 17.
Licha ya changamoto za kazi ya Urubani Koki anasema mambo bado
Babake Koki pia ni rubani. Yeye ndiye alimfanya mwanawe kupenda kuendesha ndege. Alianza kufurahia kazi hiyo kila alipomuoana babake akiifanya na hapo ndipo akaamua naye kwamba siku moja atakuwa rubani kazi inayofanywa zaidi na wanaume.
Alianza masomo yake katika chuo cha mafunzo ya uendeshaji ndege cha Oklahoma nchini Marekani.
Anasema angependa zaidi kuwasaidia wasichana wengine wa kiafrika na pia kuanzisha wakfu wake wa kuwasaidia watu masikini katika jamii.
Comments
Post a Comment