MSANII MWINGINE WA BONGO MUVI AFARIKI DUNIA

  
 Gladness Mallya

TASNIA ya filamu Bongo imepata pigo tena baada ya msanii aliyekuwa akichipukia kwa kasi, Patrick August ‘Bryton’ kufariki dunia kwa ajali mbaya ya pikipiki.Akizungumza na paparazi wetu, Mwenyekiti wa Sherehe na Maafa kwa wasanii wa Wilaya ya Kinondoni, Masoud Kaftany alisema Bryton alipata ajali usiku wa kuamkia Jumapili maeneo ya Tabata - Relini wakati akirejea kwao maeneo ya Tabata - Kinyerezi.
 
Mwili wa aliyekuwa msanii wa filamu Bongo, Patrick August, ‘Bryton’ ukiwa ndani ya gari.



Comments