Robin William ni star aliyeanza kupata mafanikio akifanya kazi kama stand up comedian na baadae kuanza kuonekana kwenye movie.
Akiwa na miaka 63 Robin amefariki dunia kwa kifo ambacho hadi sasa hakijajulikana chanzo chake lakini tetesi zinasema kuna uwezekanao kwamba Robin alijiua.
Mwili wake umekutwa nyumbani kwake huko Tiburon California na watu wa karibu wanasema alikuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo hivi karibuni.
Enzi za uhai wake aliwai kushiriki kwenye movie kama The Fisher King,Good will Hunting,Jumanji,Popeye na nyingine. Pia alishinda tuzo kama Academy,Golden Globe,Emmy,Grammy na nyinginezo kwa wakati tofauti.
Comments
Post a Comment