Staa wa Filamu za Kibongo aliyeamua kumpokea Yesu, Ruth Suka 'Mainda' amesema amekuwa akipata wakati mgumu kumjua mwanaume wa kweli ni yupi ambaye anaweza kumuoa na ndoa yake ikawa na raha badala ya majuto kama ilivyo kwa baadhi ya wasanii wenzake....
Mainda alisema hakuna kipindi kigumu kama kujua yupi ni mwanaume sahihi wa kumuoa na hili limekuwa likiutesa moyo wake japo sasa ameamua kumwachia Mungu wake ili amsaidie kwani kwa akili zake ameshindwa...
"Hakuna wakati mgumu kama kipindi cha kumpata mume sahihi kutoka kwa mungu, kwani ukijichanganya unaweza kuchukua mwanaume ambaye si wako na kusababisha kuwe na mafarakano ndani ya ndoa na hili ndio linaumiza kichwa changu kwani mpaka sasa sijajua ni yupi kati ya wengi wanaohitaji kunioa," alisema Mainda
Msanii huyo alisema anajifunza mambo mengi kupitia ndoa za watu waliomtangulia kwani nyingi zimejaa vurugu likiwemo suala la kusalitiana na kuambukizana magonjwa ya zinaa kama vile Ukimwi na menginenyo, hivyo naye hatapenda awe miongoni mwa ndoa hizo
Comments
Post a Comment