MCHUNGAJI WA BEYONCE AELEZA ANACHOJUA KUHUSU MICHEPUKO YA JAT Z NA BEYONCE

Kuna story zilisambaa baada ya ugomvi kati ya Solange na Jay Z ndani ya lift kuwa ndoa ya Jay Z na Beyonce imejaa vurugu kama uwanja wa vita na kwamba Jay Z anachepuka kivyake huku Beyonce nae akidaiwa kuchepuka na mlinzi wake.
Celebrities Attend The New Jersey Nets v New York Knicks Game - February 20, 2012
Mchungaji Rudy Rasmus wa kanisa la St. John’s United Methodist ambalo alikuwa akisali Beyonce na familia yake pamoja na rafiki yake Kelly Rowland amefunguka kuhusu tuhuma hizo na anachokijua kuhusu uhusiano huo kwa sasa.
Akkifanya interview na The Grio, mchungaji huyo ametofautiana kabisa na mawazo ya watu wengine na kueleza kuwa uhusiano kati ya wanandoa hao kwa sasa una nguvu kuliko kipindi chochote walichokuwa pamoja.
“Ni marafiki. Uhusiano wao una afya tele na maisha yao yameendelea kuwa mazuri.” Amekaririwa mchungaji Rudy ambaye pia ni mwanaharakati.
2011 NBA All-Star Game - Performances And Celebrities
Amemtetea pia Beyonce kama muumini wa dini ya kikristo kwa kile ambacho amekuwa akikosolewa na waumini wa dini hiyo kuwa anaimba nyimbo za kidunia zilizo kinyume na matakwa ya Mungu.
Amesema Beyonce ni mburudishaji na kazi yake ni kuburudisha watu. Amewashangaa wanaomponda Beyonce kwa kuwa anachokifanya ni kuburudisha tu kama anavyofanya muigizaji kama Arnold Schwarzenegger.

Comments