MASKINI BETTY KIFO CHAKE CHALETA MSHITUKO DAR NI BAADA YA KUANDIKA KAULI HII KATIKA MTANDAO WA KIJAMII
Malisa Godlisten
2 hrs ·
BEHIND THE SCENE; KIFO CHA BETTY.!
Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakubadilishi ukweli kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.
Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi watu wamesema mengi, na yameandikwa mengi. Kila mmoja kwa namna alivyoguswa. Zitto Kabwe ametweet hivi asubuhi "Justice for Betty", akitoa rai haki ipatikane kwenye kifo cha Betty.
Jokate Mwegelo nae ametweet kuomba msaada wa kuchunguza kifo cha Betty. Na watu wengine maarufu kila mmoja kasema neno, labda kwa sababu Betty alikua maarufu in one way or another.
Lakini hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake, alinyanyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo chake, lakini mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.
Saa chache kabla ya kifo chake Betty alitweet kua "PINDA HAWEZI KUWA RAIS". Baada ya kutweet hakuonekana tena hadi alipookotwa mtaroni kesho yake asubuhi akiwa amefanyia vitendo vya kikatili na akiwa amepoteza fahamu.
Lakini kabla hata ya kutweet hivyo, Betty alikua anaandamwa sana mtandaoni huko Twitter. Kuna watu walianzisha team ya kumtukana, kumjibu hovyo na kumprovoke kwa kila alilofanya.
Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu kwa Betty kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususani cha mtu maarufu.
Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki. Wanaochafua wenzao, kutishia wenzao kwa kujifanya askari JKT, kusengenya na kupost majungu.... Aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza.
Kwenye hii mitandao, matusi imekuwa njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, Facebook na Instagram lakini ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'
Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo.
Marehemu Betty ni victim wa yote hayo. Alitukanwa sana, na aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria, superstar uchwara etc.. and i hope hao waliomuita hivyo wanajifahamu na wengine wananisoma hapa.
Japo sijui chanzo cha 'ugomvi' wao, lakini naamini kuna watu wengi tu waliokuwa katika nafasi ya kuzima moto huo kwa vile walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika lakini kwa sababu ya unafiki wakapalilia moto maana wanafurahi watu wakigombana.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni UNAFIKI. Watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake.
Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa kwamba 'wakati muafaka wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.'
Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali.
Mojawapo ya Tweet za mwishomwisho za marehemu alisema hivi "Do I have a sister to support me? No. Do I have a Dad/Mom to run to or support me. No. Im hurting and wanna cry? Yes. BUT I know God is watching"
Haihitaji degree ya Saikolojia kujua kuwa Betty alikua kwenye kipindi kigumu mno na alihitaji msaada kwa watu waliokua karibu yake.
Betty anauliza"Nina dada wa kunisaidia? Hapana. Nina baba au mama wa kumkimbilia? Hapana. Nimeumizwa/nina uchungu na ninahitaji kulia (lakini nitamlilia nani?). Ila najua Mungu anaona"
Kwa bahati mbaya Betty hakuwa na baba, hakuwa na mama, hakuwa na dada wala kaka. Wote walishatangulia mbele ya haki. Alibaki peke yake, peke yake na Mungu wake.
Lakini binadamu wasivyo na aibu wala huruma wakazidi kumtukana na kumsimanga, huku wengine wakiporomosha matusi mazito. Hawakujua yaliyokua moyoni mwake. Wakamtambia kwa maisha mazuri wanayoishi na namna walivyobarikiwa.
Betty akiwa katika maumivu makali ya hisia akapost hivi "Thank you all for the names i was called, luck y'all have such a perfect life.! No hard feelings.. Im alive still.! Endeleeni kuongea"
Kwa tafsiri isiyo rasmi Betty alisema "Asanteni kwa majina yote mliyoniita. Mmebarikiwa kuwa na maisha mazuri.! Hamuumizwi na hisia kama mimi. Ila bado ninaishi, endeleeni kuongea"
Kwa bahati mbaya hakuna aliyejali, hadi juzi asubuhi (jumatano) Betty alipookotwa kwenye mtaro akiwa amefanyiwa unyanyasaji wa kijinsia na akiwa amepoteza fahamu.
Kifo cha Betty ni miongoni mwa vifo vya kikatili sana kuwahi kutokea nchini. Nashauri wanaharakati ea haki za wanawake wapambane kuhakikisha haki inapatikana. Akina Annanilea Nkya, Hellen Kijobisimba watafute haki ya binti huyu kzma Zitto Kabwe alivyosema "Justice for Betty"
Imagine mtu aliyekua kwenye maumivu makali ya hisia, anatekwa na genge la wahuni. Bila kujali kipindi kigumu alichokua anapitia, bila kujali hakua na wazazi, bila kujali psychological toacher aliyokua nayo still wanamfanyia unyanyasaji wa kijinsia hadi anapoteza fahamu.
Betty aliokotwa mtaroni na kupelekwa hospitali. Jana (alhamisi) aliweza kufungua macho, lakini hakuweza kuongea lolote hadi saa 3 usiku wa kuamkia leo, mauti ilipomkuta.
Kwaheri Betty, kwaheri classmate wangu (Majengo sec), kwaheri rafiki, kwaheri ndugu. Umeondoka dunia bado inakuhitaji. Naumia u have gone too young, lakini naumia zaidi coz umekufa kikatili mmno. Japo sijui nitakufaje, lakini nadiriki kusema hukustahili kifo cha aina hii.
Nakumbuka sms yako ya mwisho kwangu uliniambia hivi "Malisa blv me, only youths can change this country". Leo nilipopata taarifa ya kifo chako nimerudia kuisoma sms yako mara mbilimbili. Sikujua kua sms hiyo ndo ulikua unaniaga.
Umeniaga kwa kutuachia vijana wosia, kuwa vijana pekee ndio wenye uwezo wa kuibadilisha nchi hii. Nitakua nimekusaliti ikiwa sitautendea kazi wosia huu. I promise to fight and motivate other youths to liberate this country for ur dedication.
Umekwenda kumfuata mama yako, umemfuata baba yako. Wazazi wako walitangulia, leo wewe umewafuata. Hatimaye familia nzima mmekutana Paradiso.. Pumzika kwa amani Betty.!
BURIANI BETTY NDEJEMBI: TUSAKE #JusticeForBetty KWA KUPAMBANA NA UNYANYASAJI MTANDAONI (CYBERBULLYING) PIA.
Ninaandika makala hii nikitambua bayana kuwa itamuudhi kila mtu anayeingia mtandaoni kwa minajili ya kuwanyanyasa watu wengine. Lakini siku zote ninaamini katika busara hii: kuuchukia ukweli hakuufanyi kuwa uongo. Ukweli ni ukweli na uongo ni uongo. Ukweli hauwezi kuwa uongo, na kadhalika uongo hauwezi kuwa ukweli. Kamwe asilani.
Wakati tunaomboleza kifo cha ndugu yetu Betty Ndejembi hatuwezi kukwepa ukweli kwamba siku chache kabla ya kifo chake binti huyo alinynyaswa mno kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Japo hadi muda huu hatuwezi kuhusisha moja kwa moja uhusiano kati ya unyanyasaji huo na kifo cha binti huyo, ukweli tu kwamba mtu akinyanyaswa masaa kadhaa kabla ya kifo chake, waweza kujenga picha flani.
Naomba ieleweke kuwa simlaumu mtu kwa sababu sina mamlaka ya kufanya hivyo bali dhima ya makala hii ni rambirambi zangu na kuzungumzia tatizo la unyanyasaji mtandaoni, sambamba na suala zima la unafiki kila kinapojiri kifo hususan cha mtu maarufu.
Tuna tatizo kubwa huko mitandaoni. Tumefika hatua ya kuwapa umaarufu watu wenye matusi ya nguoni, wazushi, wambeya, wanafiki, wanaharamu na kila aina ya binaadamu wanaostahili laana lakini twaishia kuwatukuza. Kwa Twitter, matusi imekuwa ni njia ya mkato ya kupata umaarufu. Kuna wenzetu wengi tu wenye 'umaarufu' huko Twitter, na ukidadisi chanzo cha 'umaarufu' huo, utaambiwa 'ah huyu ana matusi si mchezo!'
Kuna watu wazima na akili zao wanatumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii aidha kunyanyasa wenzao kama si kusherehesha unyanyasaji huo. Marehemu aliitwa majina kadhaa ya kumdhihaki kabla ya kukutana na mauti. Kuna waliomwita Di Maria na wanajifahamu. Japo sijui chanzo cha 'ugomvi na aliogombana nao' (na ndio maana sikujihusisha nao kwani haukunihusu), kuna wanafiki wengi tu waliokuwa katika nafasi nzuri ya kuzima moto huo hasa kwa vile baadhi yao walikuwa wakizifahamu pande zote mbili za 'ugomvi' husika.
La kukera zaidi ambalo ni wazi litajichomoza wakati wa maombolezo haya ni unafiki: baadhi ya watu walewale waliodiriki kumwandama marehemu wakati wa uhai wake watageuka kuwa wenye uchungu mkubwa baada ya kifo chake. Hii inanikumbusha suala ambalo nimeshawahi kulizungumzia mara kadhaa, katika hali ya utani japo wenye uweli, kwamba 'wakati mwafaka kabisa wa kutafuta vipaji vya uigizaji ni kwenye misiba: watu walewale waliokuwa wakikuchukia kwa nguvu zote watageuka wenye uchungu mkubwa kwa kifo chako.
Ukiangalia baadhi ya tweets za mwisho za marehemu ni wazi kuwa binti huyo alikuwa anahitaji msaada kutoka kwa wanaomjali
ata pasi uelewa wa taaluma ya saikolojia, tweets za aina hii zinaashiria tatizo, na laiti 'wenye upendo wa dhati' wangeingilia kati muda huo, huenda muda huu Betty asingekuwa marehemu.
Na hizo tweets mbili ambazo ni miongoni mwa za mwisho kabisa za marehemu ni ushuhuda tosha wa jinsi alivyokuwa akisumbuliwa na wanyanyasaji dhidi yake mtandaoni. Ndio pengine kilichomuua ni maradhi ya kawaida ya kibinadamu lakini kila mwenye ubinadamu hatoshindwa kuhusisha unyanyasaji huu na hali mbaya ya afya aliyokuwa nayo hadi anafariki.
Kuna watakaolaumu kuwa ninatumia kifo cha binti huyo kwa 'maslahi binafsi.' Hapana, sina maslahi yoyote binafsi hasa ikizingatiwa kuwa sikuwa nikifahamiana na marehemu. Hakuna anani-follow na mie sikuwa nam-follow. Labda maslahi pekee niliyonayo ni upinzani wangu mkali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Vyovyote ilivyo, marehemu alikuwa bullied kabla hajafariki na atakayetaka kukataa ukweli huo na akatae lakini utabaki kuwa ukweli usioweza kugeuka uongo. Na kwa hakika, kila aliyeshiriki kumnyanyasa binti huyo atakuwa anasutwa na nafsi yake, hata kama atatafuta hifadhi kwenye 'huu sio wakati wa kulaumiana' au 'we failed you Betty.'
Mara nyingi nimekuwa nikiwalaumu watu wanaodai 'Instagram imekuwa mbaya' au Twitter imeharibika siku hizi' ambapo mara zote nimewakumbusha wahusika kuwa katika hii mitandao ya kijamii, ni muhimu kuwa makini katika nani wa kum-follow. Maana yangu ni kwamba ukim-follow mtu mwenye matusi, utashuhudia matusi katika anachoandika. Ukim-follow mtu wa busara, utashuhudia busara.
Hata hivyo, katika siku za hivi karibuni kumeibuka kundi kubwa tu la watu wenye busara na elimu zao lakini wepesi wa kuvutiwa na vitu vya 'kipuuzi' - umbeya, matusi, majungu, na upuuzi mwingine, na hawasiti kushea na wanaowa-follow. Ni hivi, mtu akitweet tusi, kisha ukali-retweet, utambue kuwa unalikuza (amplify) tusi hilo. Na kimsingi, kwa kiasi kikubwa, tuna-RT vitu tunavyoviunga mkono. Uki-RT tusi maana yake unaliunga mkono. Na ni wazi mwenye kujiheshimu, na kuheshimu 'watu wa maana' wanaom-follow hawezi ku-RT upuuzi.
Tatizo kubwa sasa ni kwamba waweza kuamua kuwa-follow watu unaodhani wana busara au akili za kutosha lakini ukaishia kusoma vitu vya ajabu ajabu kwenye timeline yako kutokana na haya 'mahaba' ya ku-RT vitu vya kipuuzi.
Binafsi, nadhani chanzo kikubwa cha mitandao ya kijamii kuwa 'sehemu za kukera, kuogopesha, kunyanyasana, nk' ni ile hali ya baadhi ya wenzetu kutokuwa na vitu muhimu vya kufanya katika maisha yao. Ni wazi kwamba ukiwa busy na maisha yako hutokuwa na muda wa kubughudhi wenzako.
Kingine kinachopelekea social media kuwa 'dunia uwanja wa fujo' ni ugonjwa mkubwa unawasumbua baadhi ya wenzetu: kusaka sifa wasizostahili. Wanasema,. ashakum si matusi, 'lugha ya mpumbavu ni matusi,' na ndo maana baadhi ya wenzetu wasio na cha maana cha kuongea katika hadhara hukimbili matusi, unyanyasaji, maneno macha
Nitamke bayana kuwa siandiki makala hii nikitegemea kuungwa mkono na wahusika wa unyanyasaji mtandaoni. Na kwa hakika kuna uwezekano mkubwa wa makala hii kuzua 'kampeni ya chuki' dhidi yangu kutokana na makala hii. Tatizo kubwa la wenzetu hawa ni kutotaka kuambiwa kuwa 'Hapana, hili ni kosa. Na kosa ni kosa, haliwezi kuwa sahihi.' Lakini pamoja na uwezekano wa 'kuwashiwa moto' kutokana na makala hii, wito wangu kwa kila mwenye busara na akili ni kuliangalia tukio hili la kusikitisha kama 'wake up call.' Tujifunze, tujisahihishe. Tuache kusherehesha vitu vya kipuuzi mtandaoni.
Ifike mahala, ukishindwa kumkemea mtu mwenye tabia mbaya mtandaoni basi chukua option rahisi ya kum-unfollow au ikibidi kum-block. Na ifike mahala kuwafahamisha watu wanaoendekeza utoto, majungu, umbeya, unyanyasaji na upuuzi mwingine kuwa kama hawana kitu cha maana cha kufany katika maisha yao basi isiwe sababu ya kuwasumbua wenzao wenye majukumu katika maisha yao.
Tukemee maovu badala ya kutarajia yataondoka yenyewe tu. Tuomboleze kifo cha Betty kwa kusema 'NO' kwa cyberbullies (wanyanyasaji wa mtandaoni). Tufike sehemu tuache kuwasujudia wahuni wanaodhani matusi ni sehemu ya wimbo wa taifa. Tuwakwepe waendekeza majungu, wanyanyasaji, wataka sifa za kipuuzi, na watu wasiofaa katik maisha yetu.
Wakati 'tunatafuta haki kwa marehemu Betty kutokana na unyama aliofanyiwa,' suala ambalo ni la kisheria, kilicho ndani ya uwezo wetu ni kukemea unyanyasaji mtandaoni (cyber bullying). Wakati hadi muda huu hatuwajui waliomfanyia marehemu unyama huo, takriban sote twawajua vema wanyanyasaji wa mtandaoni. Tuanze na hawa, kwani leo wamefanya kwa kwa marehemu Betty kesho itakuwa kwako.
Mwisho kabisa, ni muhimu kwetu sote kutambua kuwa tulitoka kwa udongo na tutarudi kwa udongo. Kifo ni hatma ya kila mmoja wetu.Betty ametutoka lakini nasi twaelekea huko. Visa, chuki, kunyanyasana, na vitu vingine visivyopendeza japo ni kama sehemu ya maisha yetu havipaswi kupewa nafasi katika maisha yetu haya ambayo hakuna mmoja wetu mwenye japo 'lue' ya lini yatafikia kikomo. TUPENDANE na TUHESHIMIANE.
Kwako marehemu Betty, hakuna tunaloweza kusema au kufanya sasa kurejesha uhai wako. Na hakuna neno sahihi la kuonyesha jinsi gani kifo chako kimewagusa wengi. Kubwa tunaloweza kufanya ni kukuombea kwa Mwenyezi Mungu akupatie pumziko la milele na mwanga wa milele akuangazie upumzike kwa amani. Amina.
Comments
Post a Comment