MANENO YA DIAMOND YAMCHOMA AUNTY



Star wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama rafiki wa Wema...
Diamond juzi alisema  kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa aliyonayo sasa.Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza  jana kwa sharti la kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa hata kidogo huku akibaki kuumia.

Comments