LULU AONYESHA MAPENZI YAKE YA DHATI KWA JUSTINE BIBER


Muigizaji Elizabeth Michael aka Lulu anaendelea kuonesha hisia zake kwa Justin Bieber na sasa ameeleza kuwa atakuwa anamuandikia ujumbe kila Jumatatu.
Kupitia Instagram, Lulu amepost picha ya JB akiwa kifua wazi akipiga kinanda na kuandika ujumbe akiwajibu wale wanaodai kuwa anaota ndoto za mchana na kwamba hatampata.
“Mapemaaaa...Kabla cku haijawa ngumu..! Haya ni hv wale wa kuandika ndoto za nn cjui...Mara cjui huwezi kumpata na cjui kimepanda kimeshuka...msinijazie comment😂😂😂Acha niwape ufafanuzi kdgo...ni hv Huyu Bwana swala ya yy kupenda....nimemwachia awapende kina @selenagomez na wengine wote anaotaka kuwapenda...ila swala la yy kupendwa Aniachie Mimi....yan hyo kazi yangu....!!!

Sasa Kama ni ndoto Wallah ctaki kuamka,Kama ni ufala...yani ninaukubali kwa asilimia 150%,na mengine mengine yote...sasa Kama nakuchefua,Nina uhakika Zile ndimu za @diamondplatnumz haziwezi kukutosha mana hiki kichefuchefu co cha kuisha,bora utafute mbegu ya Malimao au mbilimbi upande kwako kbsa....Na hili Zoezi ni endelevu...yani kila Jumatatu...Kama Mshahara vile....!!! #MCM...... #Nilikuwepo

Comments