Mama mmoja mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, aliyejitambulisha kwa jina la Mama Zahara, ameibuka na madai mazito akimtuhumu msanii wa filamu ambaye pia ni mjasiriamali, Lulu Mathias Semagongo ‘Anti Lulu’ kumtumia ‘SMS’ za usagaji mwanaye aitwaye Zahara ambaye ni denti wa kidato cha pili.
MSIKIE MAMA MWENYEWE
Akizungumza kwa hasira, Mama Zahara aliwaka: “Mimi nina mtoto huyu tu wa kike, anasoma boarding huko Tanga lakini hivi karibuni alirejea akidai wamepewa likizo ya wiki moja.
“Tangu huyu mtoto amekwenda boarding, nimebaini amebadilika sana, amekuwa na vijitabia ambavyo sivielewi hivyo nikawa namchunguza sana.
“Leo (Jumanne wiki hii) wakati niko jikoni nikasikia anaongea na mtu akiwa chumbani kwake, mazungumzo yale yalinitia shaka kwani kuna muda nikamsikia ‘akimkisi’ aliyekuwa anazungumza naye.
“Nilihisi kitu f’lani lakini nikasema nitamvizia nichukue simu yake nikiamini kama kuna kinachoendelea nitagundua, na kweli, alipotoka kwenda bafuni nikaichukua simu yake na kukutana na mambo ya ajabu.
“Nilinasa hizi sms ambazo zilinionesha waziwazi kwamba mwanangu anafanya vitendo vya kisagaji. Niliumia sana hasa ukichukulia kwamba nina binti huyo tu.
“Nilipoichukua ile namba, nikataka kujua kama kweli alikuwa anachati na msichana mwenzake au mwanaume, ikabidi nifanye kama nataka kumtumia pesa kwenye simu yake na hapo ndipo likaja jina la Lulu Semagongo.
“Nilishtuka kwani namjua huyu msanii tangu alipokuwa mtangazaji. Nilipompigia akanijibu kwa kifupi tu kwamba nimlee vizuri mwanangu na yeye hawezi kumfanyia vitendo hivyo, nikaona bora nije kwenu mtanisaidia.”
MESEJI ZENYEWE ZIKOJE?
Zahara: Natamani kufanya kale kamchezo, unaweza kunisaidia?
Anti Lulu: Nitumie pesa!
Zahara: Kiasi gani cha pesa? Pesa siyo tatizo, umenielewa lakini? Nataka tu…(kitendo kichafu).
Anti Lulu: Nitumie hiyohiyo, kwa muda huu nitumie 30,000.
Zahara: Sawa halafu tunaonana vipi?
Anti Lulu: Nitumie pesa muda huu, Jumamosi.
Zahara: Mbona mbali sana mpenzi, leo haiwezekani au hata kesho, pesa siyo tatizo.
Anti Lulu: Nitumie pesa basi.
Zahara: Subiri kidogo baby, simu yenye pesa iko kwenye chaji, usijali, nashukuru kwa kunionea huruma.
Anti Lulu: (kimya).
KESHO YAKE
Anti Lulu: Umeona ishu kunidanganya siyo?
Zahara: Siwezi kukudanganya mpenzi, ndiyo naamka nitakutumia ila usije ukanidanganya maana nina..., hiyo Jumamosi tunaonana wapi?
Anti Lulu: Tuta-meet (kukutana) Bondeni Hotel (ipo Magomeni, Dar), basi nitumie hiyo pesa.
Zahara: Nikutumie kwenye namba hii, vipi tutatumia vifaa?
Anti Lulu: Nitumie kwenye namba hii.
Zahara: Nijibu basi kama tutatumia vifaa au hivihivi…
Anti Lulu: Hakuna haja ya vifaa, mimi natosha…
Zahara: Haya natuma, nitafurahi sana.
Baada ya maelezo ya mama huyo kisha kuziona sms hizo, kweli zilionesha Zahara ndiye aliyekuwa akimshawishi Anti Lulu amfanyie kamchezo hako huku msanii huyo naye akionesha kuujua na kutaka apewe kwanza Sh. 30,000, Ijumaa lilimsaka Anti Lulu ili kupata maelezo yake ambapo alikuwa na haya ya kusema:
HUYU HAPA ANTI LULU
“Kusema ukweli huyo binti ndiye aliyekuwa akinisumbua kwa kunitumia sms za kunitaka.
“Alionekana kuuzoea na kuupenda sana sana huo mchezo, mimi sijawahi, ni two different things (vitu viwili tofauti).
“Inavyoonekana alitaka kunichafua kwani alinilazimisha sana, sijawahi kufanya huo mchezo na wala sifikirii hasa kwa binti kama mimi ambaye naamini wapo wanaume wanaonipenda, niingie kwenye usagaji natafuta nini?
“Huyo binti mwambieni anikome kabisa.”
Comments
Post a Comment