KUNDI LA ROCKAZ LAINGIA STUDIO BILA MO ROCKA

Quick Rocka,Chief Rocka Na Dau Rocka 
Kundi la Rockaz linaloundwa na wasanii Quick Rocka,Mo Rocka, Dau Rocka na Chief Rocka limeingia studio kwaajili ya kazi mpya. Fahamu hii ni mara ya kwanza kundi hili linafanya kazi pamoja toka mwaka 2011.

“Kundi lipo studio siku tatu mfululizo wakitengeneza nyimbo studio tofauti ambazo ni Fish Crb [Lamar], Am Records [Maneck] na Switch [Nah Reel] ,Lengo ni kujenga chemistry tena na kuwa na kazi nyingi iliwachague inatoka ipi, Pia kabla ya mwezi wa tisa wataweza kutoa Audio moja na video moja” Alisema Quick  Rocka.
Kuhusu Mo Rocka kuwepo kwenye kundi na kwenye nyimbo Quick amesema mpaka sasa  simu ya Mo Rocka haipatikani na wametumia nguvu kumtafuta bila mafanikio, wataendelea kurekodi mpaka akipatikana atafanya sehemu yake.

Comments