Siku ya jana haikua nzuri kwa Shilole na Nuh Mziwanda
baada ya kugomabana sana hadi Nuh Mziwanda akaamua
kuchukua vitu vyake na kuhama Kwa Shilole, Gazeti la
Makorokocho imezipata taarifa hizi za motomoto kupitia
kwa mtu
aliyekuepo eneo la tukio aliyedai kuwa yeye alishangaa
kuskia mikikimikiki ndani ya Harrier na baadae milango ya
gari ikafunguliwa wakatokeza wasanii wawili wa bongo flava
ambao ni Shilole na Nuh Mziwanda na walikua
wakirushiana maneno ghafla wakatokeza watu
wengine wakiongozwa na Msanii Chege
Chigunda wakaamulizia ugomvi huo bila Mafanikio
kwani Nuh Mziwanda alikua anamuambia Shilole
amrudishie simu yake lakini Shishi alishindwa kufannya
hivyo kwa madai eti ufunguo upo nyumbani, Kweli? wakati
dakika chache zilizopita walikua ndani ya Gari.
Nilipomtafuta Nuh Mziwanda hakutaka kubisha na akatiririka
A to Z ya sakata hilo, Nuh Mziwanda: Jana Usiku tulialikwa
Chakula Usiku kwa Producer Dibanjo, mitaa ya
Mango Garden Kinondoni, mimi na Shilole tulipofika
pale tukamkuta mwenyeji wetu pamoja na wasanii wengine
Chege, Julio, Dully Sykes na wengine, ikafika muda nikawa
sijiskii vizuri nikamuomba Shishi funguo ya gari ili
nikapumzike kwenye gari, kufika kule nikazikuta simu za
Shilole zikiwa na missed call nyingi pamoja na msg,
nikazikagua na kukuta msg ya mwanaume akimwambia
Shilole "Nimeingia Dar" .... ikabidi nimuite Shilole
na kumkaripia sana Shishi akajitetea kuwa yule si bwana
wake, Nikamwambia sawa mpigie niskie maongezi yenu,
lakini Shishi alipompigia sikuelewa maongezi ndo
nikamzaba kibao cha nguvu na Shishi akajibu mapigo kwa
kuning'ata mwilini pamoja na kidole changu
kimevimba mpaka wakati huu, watu wakajaa eneo la
tukio hadi kina Chege wakafika na kuanza kuamulizia
kupigana lakini mwisho wa siku Shilole alikua amenipokonya
simu yangu nilipomuomba akakataa kuirudisha na kuondoka eneo la tukio,
Ikabidi na mimi nisepe kwenda Nyumbani kwa Shilole
ambako nilikua naishi nae ila nia yangu ilikua ni kwenda
kuchukua vitu vyangu ili nihame nyumba ile, njiani karibu
nafika nikakutana na vibaka wakaniibia mpaka viatu,
nikaendelea na safari lakini nilipofika pale kumbe Shishi
alikua amempigia simu Dada wa Kazi asinifungulie mlango,
ikabidi nikae hapo nje weeee mida mida Shilole akafika na
kupitiliza ndani akajifungia mimi nikiwa nje, asubuhi
wakajisahau na kuacha mlango wazi ndipo nilipopata
upenyo nikaingia na kuchukua laptop, guiter pamoja na
nguo vyote vyangu na kumwachia nyumba yake.
Comments
Post a Comment