Kuna ile stori ya Watoto wawili mmoja miaka 10 na mwingine 7 wote kutoka wilayani Hanang mkoani Manyara ambao walikua wanatuhumiwa kumuua mwenzao wa miaka mitatu kwa kumchapa na kisha kumnyonga, ilikua taarifa kubwa sana ndani ya wiki nne zilizopita.
Baada ya kushikiliwa kwa muda, watoto hawa wameachiwa huru ambapo gazeti la Mwananchi limeripoti.
Alichosema Mwanasheria ni kwamba watoto hawa wameachiwa huru kutokana na umri wao kuwa mdogo na kushindwa kutambua zuri na baya.
Comments
Post a Comment