Mzungu aliyekuwa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’ anadaiwa kuingilia penzi la mwigizaji Wema Sepetu.
Ishu hiyo imebumburuka ikiwa ni siku chache tangu Diamond atangaze kuwa hayupo tayari kuoa akidai atashuka kimuziki.
Ishu hiyo imebumburuka ikiwa ni siku chache tangu Diamond atangaze kuwa hayupo tayari kuoa akidai atashuka kimuziki.
Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Zdravko Logarusic ‘Loga’ akipata ukodaki na Wema Sepetu ndani ya ofisi za Global.
KUMBE ALIMZIMIA KITAMBO
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mcroatia huyo alimzimia Wema mara tu baada ya kutua nchini Desemba, mwaka jana na kumuona mlimbwende huyo ‘akishaini’ kupitia vyombo vya habari, akajiwekea nadhiri kwamba lazima ampate.
CHANZO CHATIRIRIKA
“Loga alimzimia kinoma Wema baada ya kumuona kwenye vyombo vya habari na kuanza kufuatilia baadhi ya filamu zake ambazo zilikuwa zilimkonga moyo kila alipozitazama.
“Baada ya kuvutiwa naye, mtu mzima (Loga) akaanza kutafuta mbinu za kumuimbisha Wema,” kilidai chanzo.
Chanzo hicho kilidai kwamba baada ya kocha huyo kupata wazo la kumtongoza Wema, alianza kumsaka katika viwanja ambavyo aliamini mrembo huyo anatembelea ili aweze kufanikisha azma yake ya kuonja penzi la Beautiful Onyinye.
Zdravko Logarusic ‘Loga’akiwa kazini.
AMSAKA NYUMBANI KWAKE
Ilisemekana kuwa mara kadhaa alishafanya jitihada za kumfuata Wema nyumbani kwake Kijitonyama jijini Dar lakini kila alipotia mguu, hakufanikiwa kuonana na mrembo huyo.
Hata hivyo, ilisemekana kwamba Loga hakukata tamaa kwani alionekana kudata kadiri siku zilivyozidi kuyoyoma.
“Jamaa alipiga sana misele pale Kijitonyama lakini bahati mbaya, misele yake haikuzaa matunda lakini kwa kuwa alikuwa na nia, hakukata tamaa, aliendelea kumsaka katika viunga mbalimbali ambavyo aliamini Wema yupo,” kilidai chanzo hicho.
ZALI LA MENTALI
Kikizidi kumwaga taarifa, chanzo hicho kilibainisha kuwa jitihada za Loga kukutana na Wema zilizaa matunda Aprili 22, mwaka huu maeneo ya Mwenge ambapo bila kutegemea, wawili hao walikutana kila mmoja alipokuwa katika mizunguko yake ya kikazi.
“Ilikuwa kama zali tu siku hiyo, Wema alikuwa katika ofisi moja hivi ambayo alikuwa akifanya shughuli zake za kikazi lakini wakati huohuo Loga naye alitia timu katika ofisi hiyo kwa shughuli zake za kikazi ndipo ilipokuwa golden chance,” kilizidi kudai chanzo hicho ambacho ni mtu wa karibu wa Wema.
NDOTO ZAANZA KUTIMIA
Chanzo hicho kilizidi kutiririka kuwa, mara baada ya wawili hao kukutana, pointi ya kwanza muhimu kwa Loga ilikuwa ni kubadilishana namba na mrembo huyo kisha kufanya naye mazungumzo ya kawaida kwa dakika kadhaa.
Ilisemekana kwamba, siku hiyo Loga alionekana mwenye furaha kwani licha ya kubadilishana namba za simu, ilielezwa kuwa walipata fursa ya kupiga picha za pamoja na kutumiana kupitia simu zao hivyo ukaribu wao kuanza kushamiri kuanzia hapo.
AANZA KUIMBISHA
Ilidaiwa kuwa kitendo cha kocha huyo kupata namba ya Wema ilikuwa bahati kama kuokota madafu kwenye miti ya miembe, haraka alianza kutuma maombi ya penzi pasipo kufunguka moja kwa moja kisha badaaye alifunguka kabisa.
“Alianza kwa salamu, akawa anachombezachombeza na maneno ya mitego ambayo mtu mzima ukitumiwa meseji kama hizo unajua kabisa kuna kitu mtu anakitaka kutoka kwako.
“Alipoona Wema haelekei mtegoni, akaamua bora kufunguka laivu, akamtumia meseji zinazoeleza hisia kali ya mapenzi,” kilidai chanzo hicho.
USHAHIDI HADHARANI
Ili kuupata ukweli wa madai hayo, paparazi wa Risasi Jumatano alianza kuchimba undani wa sakata hilo ambapo kwa kutumia njia za ‘kiintelejensia’, alifanikiwa kunasa meseji (SMS) zilizotoka kwa Loga kwenda kwa Wema ambazo zilionesha dhahiri kwamba kocha huyo amedatishwa na staa huyo wa filamu na kuomba hifadhi ya kimalovee.
Meseji hizo zilikuwa zikisisitiza kwamba Loga anamhitaji Wema lakini mtoto wa kike alikuwa mzito kumkubalia mzungu huyo ambaye sasa amesitishiwa ajira yake na uongozi wa Msimbazi, mwishoni mwa wiki iliyopita kutokana na makosa mbalimbali.
WEMA ANASEMAJE
Ili kujiridhisha zaidi, paparazi wetu alimvutia waya Wema na kumuuliza kuhusiana na uhusiano wake na kocha huyo.
Paparazi: Tumesikia Loga anakuimbisha, vipi umemkubalia au vipi?
Wema: Mh! Nani kakwambia?
Paparazi: Nijibu swali langu maana hata ushahidi wa meseji alizokutumia akionesha anakuhitaji, tumeziona na tunazo.
Wema: Kwani kuna tatizo akinihitaji? Si mwanaume, ana haki ya kupenda kama walivyo wengine lakini ishu ni kumkubalia.
Paparazi: Kwa hiyo wewe umemkubalia?
Wema: Aaaa wapi, sipo interested na wazungu hata kidogo by the way mimi nina baby wangu Diamond.
MADAI MENGINE
Wakati huohuo, mtu wa karibu na kocha huyo amepenyeza madai kuwa Loga alipanga kumhamisha Wema na kwenda kuishi naye nje ya nchi lakini haikujulikana mara moja kwamba ni nchi gani achilia mbali kama ilikuwa ni ‘gia’ ya kumpata mwigizaji huyo.
Alipotafutwa Loga ili kuzungumzia madai hayo, hakupatikana mara moja hivyo jitihada zinaendelea, tega sikio kwenye magazeti ya Global.
Kama hiyo haitoshi, pia Loga anadaiwa kutoka na mwigizaji Yvonne-Cherry Ngatwika ‘Monalisa’, madai ambayo mwigizaji huyo ameyakanusha vikali.
Source: GPL
Comments
Post a Comment