KOCHA Mkuu wa Simba, Mcroatia Zdravko Logarusic, amesema, mlinda mlango wake, Ivo Mapunda, ndiyo namba moja na Hussein Sharrif ‘Casillas’ anatakiwa kulazimisha na kumpa changamoto mwenzake ili apate nafasi ya kucheza.
Simba imemnunua Casillas ambaye ni Kipa Bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita kutoka Mtibwa Sugar ili asaidiane na Ivo ambaye msimu uliopita, alimweka benchi Mghana Yaw Berko hadi akaondoshwa kwao bila kuongezewa mkataba mpya.
Loga alisema: “Ivo ndiyo kipa namba moja wa Simba, Casillas amekuja Simba ili kuweka changamoto.
“Hivyo Casillas anatakiwa kufanya juhudi na kulazimisha namba kwa nguvu kwa kumpa changamoto Ivo ndipo aweze kucheza.”
Casillas alikuwa kipa namba moja wa Mtibwa, lakini sasa atakabiliana na changamoto ya kupata nafasi ya kucheza kwa sababu hajahakikishiwa namba hadi sasa.
Hiyo si mara ya kwanza kwa Casillas kukumbana na changamoto hiyo kwani hadi kuchukua namba moja wa Mtibwa, aliwekwa benchi muda mrefun na na Shaaban Hassan ‘Kado’ hadi kipa huyo alipoondoka kwenda Yanga, ndiyo Casillas akatawala langoni.
Comments
Post a Comment