KIUNGO wa Simba, Shaban Kisiga, ametamka kuwa Kocha Mkuu Zdravko Logarusic ni mkali wa kupindukia, lakini ukali wake ni wa kutaka mchezaji afanye kile anachokitaka kocha huyo.
Mchezaji huyo mzoefu amekiri kwamba hakuwahi kuona mazoezi kama ya Loga siku za nyuma.
Kisiga alisema: “Mwalimu ni mkali sana, lakini naamini najifunza kufuata maelekezo yake na kufanya kile anachokitaka. Ananipa vitu vipya na maelekezo mazuri na hii ninaona anakifanya kwa sisi wote watatu wakiwemo Maguli na Kwizera. Ki ukweli mpaka sasa kuna vitu vipya ninavyovipata ambavyo sikuwahi kuwa navyo.”
Katika mazoezi ya juzi Jumatano, Logarusic aliwaita mara kwa mara wachezaji Kisiga, Pierre Kwizera na straika Elius Maguli na kuwapa maelekezo, lakini pia kocha huyo alionekana akiwapigia kelele akiwataka wafuate kwa umakini maelekezo aliyokuwa akiwapa. Kisiga alisajiliwa Simba akiwa mchezaji huru akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro na amekuwa akipewa majukumu ya kiungo mshambuliaji kwenye mazoezi ambayo yamekuwa yakiendelea kwenye Uwanja wa Boko, jijini Dar es Salaam.
Comments
Post a Comment