Wakazi wa Mbeya wanatarajia kulishuhudia kwa mwaka mwingine tena joto la Kili Music Tour, Jumamosi hii, Agosti 9. Kinachofurahisha zaidi ni kuwa wasanii wengi watakaotumbuiza kwenye show hiyo wana nyimbo mpya na kali ambazo wakazi wengi wa Mbeya hawajazishuhudia zikitumbuizwa live.
AY anahit na ngoma yake ‘Asante’, Mwana FA akitamba na ngoma yake ‘Mfalme’ aliyomshirikisha Gnako na Izzo Bizness akiwa na wimbo mpya kabisa, ‘Walalahoi’ huku Weusi wakifanya vizuri na ngoma ya pamoja ‘Gere’ bila kusahau ngoma binafsi ya Nick wa Pili ‘Staki Kazi’ na ‘I See Me’ ya Joh Makini.
Kwa upande wake wa Professor J, atawapa wakazi waMbeya ladha ya live ya nyimbo zake mbili mpya, ‘Kipi Sijasikia’ na ‘Tatu Chafu’.Wasanii wengi watakaotumbuiza ni pamoja na Shilole, Rich Mavoko na Chibwa.
Kwa mara nyingine tena Kilimanjaro Premium Lager inaileta kwako Kili Music Tour 2014 katika viwanja vya New City Pub, Jumamosi Agosti 9. Ni kwa kiingilio cha buku 3 tu huku mlangoni ukipata Kili ya bure.
Comments
Post a Comment