JIDE AIKIMBIA NYUMBA


Nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’.
 NYOTA wa muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ ambaye hivi karibuni ndoa yake iliripotiwa kuwa katika sintofahamu na kuvunjika, anadaiwa kuhamia katika hoteli moja yenye hadhi ya nyota tatu iliyopo Oysterbay jijini Dar.Kwa mujibu wa chanzo chetu, Jide amekuwa akionekana akiingia na kutoka kwenye hoteli hiyo huku nyumba yake iliyopo Kimara-Temboni, Dar ikiwa haina mkazi wa kudumu.
Wiki iliyopita, kulienea taarifa katika mitandao ya kijamii ikieleza kuvunjika kwa ndoa ya Jide na mume wake, Gardner Gabriel Fikirini Habash. Wawili hao walifunga ndoa mwaka 2005.

Taarifa zikadai kwamba Gardner naye aliondoka nyumbani  hapo na kwamba hivi sasa anaishi kwa mmoja wa ndugu zake.

Comments