HUU NDO UJUMBE WA DIAMOND ALIOWAJIBU MASHABIKI WA WEMA

Diamond
Baada ya kuwa natetesi kuwa Wema na Diamond wamegombana na wanaelekea kuachana, pamekuwa na makundi ya mashabiki wanaobishana kuhusu wapenzi hawa, mashabiki wa Wema wakitaka Diamond amrudie na kumuomba msamaha kuhusu kauli yake ya kutokuwa na mpango wa kumuoa.

Diamond ameweka ujumbe huu mrefu Instagram
“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe… Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi…. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo!….Mxieeeeeeeew!

Comments