FAHAMU MASTAA 9 WALIWAHI KUDATE NA KIM KARDASHIAN

Mwanamitindo Kim Kardashian ambaye hivi karibuni ameamua kuingia rasmi kwenye game la muziki kibiashara alifunga ndoa na Kanye West May 24, mwaka huu huko Italia.

Kim Kardashian
Hata hivyo, kumekuwa na maelezo mengi ya watu kuhusu historia yake katika maisha ya mapenzi.
Hotmixmziray.com imeamua kukumbushia maisha ya mapenzi ya Kim Kardashian hasa kwa watu maarufu aliowahi kutoka nao.

TJ Jackson
TJ na Kim
Inaelezwa kuwa TJ Jackson ambaye ni mpwa wa Michael Jackson ndiye star wa kwanza kuwa na uhusiano na Kim Kardashian.

Damon Thomas
Damon Thomas
Huyu ni producer wa muziki ambaye aliwahi kufunga ndoa na Kim Kardashian na kudumu kuanzia mwaka 2000 hadi 2004.

Nick Canon

Nick Canon
Nick Cannon aliwahi kuwa mpenzi wa Kim Kardashian na mapenzi yao yalidumu kwa mwaka mmoja tu, 2006 hadi 2007.

The Game
The Game
Wengi walikuwa hawafahamu kama The Game aliwahi kuwa na boyfriend wa Kim Kardashian hadi hivi karibuni alipoamua kufunguka ukweli wakati anashambuliwa kwa tetesi kuwa anatoka na Khole Kardashian. Akana na kudai kuwa aliwahi kuwa na uhusiano na Kim K na sio Khole K.

Ray J
Ray J
Uhusiano kati ya Kim Kardashian na Ray J ulivuma sana huenda kuliko aliwahi kutoka nao kabla, na ulivumishwa zaidi na filamu fupi ya ngono waliyorekodi (Ray J na Kim Kardashian). Na hata alipoanza uhusiano na Kanye West, Ray J aliiachia wimbo wa I Hit It First uliotafsiriwa kama diss kwa Kim Kardashian na Kanye kwamba yeye ndiye aliyeanza.

Reggie Bush
Reggie Bush
Huyu ni star wa mpira wa kikapu, ambaye Kim Kardashian alidumu nae kidogo kwenye uhusiano

MileS Austin
Miles Austin
Baada ya kumalizana na Reggie Bush, Kim Kardashian alianguka kwenye mikono ya Miles Austin

Kris Humphries

Kris Humph

Kim Kardashian alitekwa na Kris Humphries kimapenzi na kuamua kufunga nae ndoa, lakini ndoa yao ilidumu kwa muda wa siku 72 tu kabla hawajatengana.

Kanye West

kanye na Kim Kardashian 
Moyo wa Kim Kardashian ulitua kwa Kanye West na wakashibana vyema hadi kumzalia mtoto wa kike, na mwisho wa siku wakafunga ndoa. Je, safari yake itakuwa imeishia kwa Kanye West? Au bado picha linaendelea kama J’Lo? Who Knows…? All the best Mrs. West.

Kanye, Kim na mtoto

Comments