AY amedai kuwa kuwa yeye na Diamond watahakikisha Chidi Benz anasimama vizuri baada ya kuyumba hapo awali.
AY ameiambia Hotmixmziray kuwa kama ilivyo kawaida yake kumsaidia msanii mmoja kila mwaka, mwaka huu atahakikisha Chidi anakaa pazuri.
“Huwa nina uhakika wa kufanya comeback nzuri tu, sio kwamba ninavyomsupport Chidi tunapata faida yoyote. Kila mwaka huwa ninampick mtu mmoja, so mimi na Diamond tuliamua kuwekeza kwenye audio pamoja na kufanya naye video pamoja kwa gharama zetu sisi. Kama unavyoona promotion yake, mpaka sasa hivi tupo kwenye process ya kufanya video. Bado hatujajua tutafanya wapi video ila tupo kwenye maandalizi ya mavazi, location na mambo mengine,”amesema AY.
Hivi karibuni Chidi Benz alitoa wimbo ‘Mpaka Kuchee’ aliowashirikisha AY na Diamond.
Comments
Post a Comment