Joto la ushindani kati ya wasanii wa Tanzania linazidi kupanda huku mashabiki na vyombo vya habari wakidaiwa kuchochea kuni kwa namna moja au nyingine.Diamond Platinumz ambaye ndiye msanii anaekabiriwa na ushindani mkubwa zaidi kwa sasa kwa kuwa yuko mstari wa mbele zaidi wa mafanikio katika muziki hapa nchini na kuvuka mipaka kuiwakilisha Tanzania, amewashauri wasanii wanaotaka kushindana nae kutojikita katika ushindani wa nyumbani.
Diamond alifunguka katika mahojiano aliyofanya na The Jump Off ya 100.5 Times Fm na Jabir Saleh kabla hajapokea tuzo ya AFRIMMA kama mwimbaji bora wa kiume Afrika Mashariki.
“Tutanue mawazo, tuache mawazo ya kushindana wenyewe kwa wenyewe Tanzania. Labda kuleta mabadiliko yataleta mabadiliko ya Chalinze, mababadiliko ya Dar es Salaam au wapi. ‘Tukakomeshana tukikutana kwenye show labda ya Mwembe Yanga,’ tuache hizo fikra.” Alisema Diamond.
Comments
Post a Comment