CRISTIAN RONALDO AMFUNIKA LIONEL MESSI KWENYE REKODI NYINGINE YA MAGOLI HUKO ULAYA

two-tiger-ronaldo-vs-messi-pics Upinzani wa wachezaji bora wa kizazi hiki cha soka Cristiano Ronaldo na Lionel Messi umekuwa ukitawala vypmbo vya habari kila kukicha.
Usiku wa jana kulikuwa na mchezo wa UEFA Super Cup kati ya mabingwa wa UEFA Europa League – Sevilla dhidi ya mabingwa wa UEFA Champions League – Real Madrid, mchezo amba ulipigwa jijini Cardiff, Wales.
Matokeo ya mchezo huo ni ushindi wa 2-0 kwa Real Madrid, Cristiano Ronaldo akifunga magoli yote mawili na kuandika rekodi nyingine kwenye soka barani ulaya.
Magoli hayo ya Ronaldo yamemfanya atimize jumla ya magoli 70 kwenye michuano ya ulaya na hivyo kumpita Messi ambaye ana jumla ya magoli 68.
Mpaka kufikia April 2012, nahodha wa Ureno alikuwa nyuma kwa magoli 18 kumfikia Messi, lakini ndani ya misimu miwili amefanikiwa kumfikia Messi na kumpita akifunga jumla ya mabao 29 ndani ya msimu miwili.
Ronaldo sasa anakuwa amefunga magoli 68 kwenye ligi ya mabingwa wa ulaya na mawili kwenye Super Cup, jumla 70, akiwa amemfikia nyota wa zamani Juventus na AC Milan Fillipo Inzaghi.
Gwiji wa soka wa Real Madrid ndio mchezaji anayeongoza kwa magoli mengi barani ulaya akiwa ameziona nyavu mara 76.

Comments