Msanii wa muziki wa kizazi kipya Bongo, Baby Joseph Madaha amenusurika kubakwa nchini Kenya baada ya kupanda jukwaani akiwa ametinga kivazi cha nusu utupu.
Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu.
“Nusura Baby Madaha abakwe, wanaume wakware walishindwa kuvumilia, palepale jukwaani wakaanza kumvuta huku wengine wakimng’ang’ania paja lake lakini aliokolewa na mabaunsa vinginevyo tungekuwa tunaongea mengine,” kilisema chanzo.
Mpekuzi imezinasa picha kadhaa zinazomuonesha Baby Madaha akiwa anang’ang’aniwa na wanaume tofauti huku wengine wakimchungulia sehemu zake ‘muhimu’ pamoja na kumshika mapaja yake.
“Kweli ilikuwa ni hatari siku hiyo maana wanaume waliniganda balaa kila nilipokuwa naimba jukwaani walikuwa wakinivutia kwa huku chini walikokuwa wamesimama lakini niliokolewa na mabaunsa, hata hivyo shoo ilikuwa na mzuka sana,” alisema Baby Madaha.
Kwenye shoo hiyo iliyokuwa na nyomi ya kutosha, Baby Madaha alikamua vilivyo sambamba na wasanii wakali kutoka Kenya akiwemo Jua Kali na Wayree.
Baby Madaha akifanya shoo na kunengua jukwaani akiwa ametinga sketi fupi.
Baby Madaha akipata akiwa na baadhi ya mastaa kutoka Kenya.
Comments
Post a Comment