AZAM FC YAWATISHIA VIGOGO WA KOMBE LA KAGAME

 

AZAM FC imepata sare ya usiku katika mchezo wake wa juzi Jumanne dhidi ya Atlabara ya Sudan Kusini, lakini timu yenye mashabiki wengi katika Kombe la Kagame, Rayon Sport, imeihofia Azam.

Akizungumza na Mwanaspoti Kocha Mkuu wa Rayon, Francois Luscioto, alisema kesho Ijumaa watashuka uwanjani kusaka pointi tatu dhidi ya KMKM ya Zanzibar, lakini tishio kwao katika kuchukua ubingwa huo ni Azam.

“Mpaka sasa tunazipa heshima kubwa timu zote lakini hawa Azam ndiyo tunaowaangalia kwa tahadhari kubwa, ni timu nzuri inayoundwa na wachezaji wazuri,” alisema Luscioto.

“Tulitoka nao suluhu katika mchezo wa ufunguzi, lakini huwezi jua tunaweza kukutana nao huko mbele, tunawaheshimu lakini hatuwaogopi.

“Wanaonekana wanaweza kufika mbali, tutajitahidi kushinda kila mchezo ili tuweze kuchukue kombe hili.”

Comments