AZAM FC WAKO VIZURI

IMG_6447.JPG
Klabu ya Bingwa ya Vodacom Premier League, Azam FC leo hii imeshuka dimbani mjini Kigali Rwanda kuiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kombe la Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Adama City ya Ethiopia.
Mchezo huo wa hatua ya makundi uliopigwa kwenye uwanja wa Nyamirambo umeisha kwa ushindi mnono kwa Azam FC.
Mabao ya Nahodha John Bocco, Mcha Viali, Didier Kavumbagu na Kipre Tchetche yameipa Azam ushindi wa 4-1.
Kwa matokeo hayo Azam inaongoza lake na imefanikiwa kutinga robo fainali ambapo itacheza na El Marreikh ya Sudan Agosti 20.

Comments