Meneja wa ziara ya magwiji wa Real Madrid Dennis Ssebo aliwaambia leo waandishi wa habari pale New Africa Hotel iliyopo posata kuwa mbali na Vodacom kuwa mdhamini mkuu ila wapo wadhamini wengine kama Fastjet,Efm Radio,Tropical,Pembe Flower,Lake Gase na Ladger Plaza Bahari Beach.
Meneja wa ziara hiyo Dennis Ssebo (katikati)akiwa na wageni.
Wachezaji hao wanatakiwa kuingia nchini agosti22 kwa ajili ya mechi ya kirafiki na wachezaji nyota wa Tanzania.Pia watafanya ziara ya kitalii kwa kupanda Mlima Kilimanjaro,kutembelea vivutio vya utalii.Miongoni mwa wachezaji watakaokuja ni miongoni mwa mchezaji bora wa zamani wa dunia wa Ufaransa Zinadine Zidane,Mreno Luis Figo,na Mbrazil Ronaldo Lima.
Magwiji hao wa Real Madrid washafanya matangazo ya kutosha ya ziara yao hiyo na wana hamu ya kukanyaga ardhi ya Tanzania.
Comments
Post a Comment