Msanii huyo anatafutwa kwa shutuma za kushindwa kutokea kwenye show aliyokuwa amesaini mkataba huko Mombasa, Kenya. Mr. Blue alikuwa anatakiwa kutumbuiza kwenye maeneo ya Office Restaurant, Likoni na Mariakani Jubilant Hotel, November 16 na 17.
Mratibu wa show hiyo, Sammy Ondwar Onyango, aliamua kwenda kushtaki polisi sababu anadai alikuwa ameshamlipa msanii huyo sehemu ya malipo waliyokuwa wamekubaliana.
“Mr Blue si mtu mwaminifu kabisa. Aliwahi kuniangusha pia mwaka 2012 kwenye show ya Jet Bar, Likoni, baada ya kudai kuwa alikosa basi ya kwenda Mombasa na nililazimika kuingia zaidi mfukoni kumlipia basi jingine,” Onyango aliliambia gazeti la The Star.
Promota huyo amesema kwenye tukio la sasa, walikubaliana kumlipa shilingi 100,000 (za Kenya) ambazo ni sawa na shilingi milioni 1.8 na tayari alikuwa ameshamlipa shilingi 40,000 kupitia M-Pesa.
Kesi hiyo imeripotiwa kwenye kituo cha polisi cha Likoni.
Gazeti hilo limesema baada ya kuwasiliana na Mr Blue kwa simu, aliweza kujibu kwa ujumbe mfupi wa simu kwamba alikuwa akiendesha gari na simu haikupatikana tena.
Comments
Post a Comment