Matokeo ya uchaguzi wa Marekani 2020: Juhudi za timu ya Trump za kupinga matokeo ya Pennsylvania zagonga mwamba

 


Mahakama moja huko Pennsylvania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na timu ya Trump inayopinga matokeo ya uchaguzi ambayo ilikuwa inataka kura zilizopigwa kwa njia ya posta katika jimbo hilo zifutiliwe mbali.

Jaji Matthew Brann alisema kesi hiyo ambayo imeegemea wizi wa kura haikuwa na "msingi wowote".

Hatua hiyo inawezesha rais mteule kuidhinishwa kuwa mshindi wa jimbo la Pennsylvania wiki ijayo ambaye anaongoza kwa zaidi ya kura 80,000.

Hili ndio pigo la hivi karibuni kwa Donald Trump ambaye anajaribu kupinga matokeo yanayoonesha kuwa alishindwa katika uchaguzi mkuu wa Novemba 3.

Bwana Trump amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi huo kwa madai kwamba kulikuwa na wizi wa kura bila ya kutoa ushahidi wowote.



Comments