Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 09.07.2020: Godfrey, Havertz, De Bruyne, Hojbjerg, Garcia

Jack Grealish
Mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish

Ajenti wa mchezaji wa Aston Villa Jack Grealish, 24, anasema kwamba kiungo huyo wa kati hajafikia makubaliano ya kujiunga na Manchester United huku klabu hiyo ikimwekea thamani ya £80m. (Metro

Klabu ya Norwich City imeitisha dau la £50m ili kumuuza beki Ben Godfrey, 22, huku klabu za Borussia Dortmund na RB Leipzig zikiwa miongoni mwa klabu zinazomwania mchezaji huyo wa timu ya England ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 21. (Sky Sports)

Winga wa Ujerumani Kai Havertz yuko tayari kuwasilisha ombi la kutaka kuhama klabu ya Bayer Leverkusen baada ya kuiambia Chelsea anataka kujiungana nayo mwisho wa msimu huu. (Star)

Kai Havertz
Winga wa Ujerumani Kai Havertz yuko tayari kuwasilisha ombi la kutaka kuhama klabu ya Bayer Leverkusen

Chelsea inatumai itachukua fursa hiyo ya Havertz ambaye atajiunga na mchezaji mwenza wa Ujerumani Timo Werner, 24, na Antonio Rudiger, 27, katika uwanja wa Stamford Bridge. (Telegraph)

Wakala wa kiungo wa kati wa Man City Kevin de Bruyne amepuuzilia mbali madai kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 na raia wa Ubelgiji anatarajiwa kuondoka Manchester City ili kujiunga na Real Madrid au Paris St-Germain. (Sporza, via Star)

Ajax imejiunga na Tottenham katika harakati za kumsaini kiungo wa kati wa Southampton na Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg, 24, huku Everton ikivutiwa na mchezaji huyo. (Telegraph)

Pierre-Emile Hojbjerg
Ajax na Tottenham zinamsaka kiungo wa kati wa Southampton na Denmark, Pierre-Emile Hojbjerg

Mchezaji mwenza wa zamani wa winga wa Brentford na Algeria Said Benrahma, 24, amempongeza winga huyo kwa kujiunga na Chelsea katika mtandao wa Instagram - akidai kwamba makubaliano yameafikiwa kati ya Chelsea na mchezaji huyo mwenye thamani ya zaidi ya £30m. (Sun)

Manchester City ina matumaini kwamba beki Eric Garcia, 19, atasalia nao huku kukiwa na mazungumzo kwamba anaivutia klabu yake ya zamani ya Barcelona. (Manchester Evening News)

Aaron Ramsey
Mchezaji wa kimataifa Wales Aaron Ramsey

Juventus imeipatia Chelsea ofa ya wachezaji wawili, ikiwemo mchezaji wa Wales Aaron Ramsey, 29, ili kubadilishana na kiuongo wa kati wa Itali Jorginho, 28. (Express via Tuttosport)

Manchester United inamchunguza beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake, 25, beki wa Aston Villa na England Tyrone Mings, 27 na beki wa AC Milan na Italy Alessio Romagnoli, 25, kama chaguo la kushirikiana na beki wa kati Harry Maguire katika safu ya ulinzi ya kati. (ESPN)

Nathan Ake
Beki wa Bournemouth na Uholanzi Nathan Ake

Hatahivyo mkufunzi wa United Ole Gunnar Solskjaer amejiondoa katika madai hayo ya kutaka kumnunua Ake ama beki mwengine yeyote wa kati. (Metro)

RB Leipzig imeziba pengo la mchezaji wao anayeelekea Chelsea Timo Werner, 24, ambaye nafasi yake imechukuliwa na mshambuliaji wa Red Bull Salzburg na mchezaji wa Korea Kusini Hwang Hee-chan, 24. Beki wa Ujerumani Benjamin Henrichs, 23, pia anaelekea kujiunga na klabu hiyo ya Bundesliga kwa mkopo kutoka Monaco (ESPN).

Timo Werner
RB Leipzig imeziba pengo la mchezaji wao anayeelekea Chelsea Timo Werner

Sheffield United inapanga kuwasilisha dau la £10m ili kumnunua beki wa Norwich Todd Cantwell, 22. (Star)

Sevilla inapanga kumnunua beki wa Arsenal na Uhispania Hector Bellerin, 25, mwisho wa msimu. Juventus na Inter Milan pia zinamnyatia mchezaji huyo. (Express)

Comments