Mh.Hamis Kigwangalla Asema Neno Baada Ya Kuona Unyama Aliofanyiwa

Hamisi Taletale hamisi kigwangalla
Mh Hamis Kigwangalla amepost ujumbe mzito baada ya kuona picha zinazoonesha mateso aliyokuwa akifanyiwa Shilole na mume Uchebe .

 @shilole  amefanya nini kinachostahili kipigo chote hiki? Hivi mwanaume ukiishampiga hivi mkeo utaweza kumuambia tena ‘nakupenda’? Na kumuita tena ‘honey’ , ‘love’, ‘lawalawa’, nk?! Unavyompiga hivi unakuwa umepeleka wapi upendo, huruma, ubinadamu na uanaume wako? Hakuna kosa linaloweza kuhalalisha kipigo kwa mkeo cha namna hii. Hakuna. Labda kama utuambie kwamba aliyetoa kipigo hiki ana aina mojawapo ya ugonjwa wa akili na amesahau kunywa dawa zake siku hiyo. Si vingine. Wanaume tuna wajibu wa kuwapenda, kuwahurumia na kuwahudumia wake zetu. Tutimize wajibu wetu huu siyo vinginevyo. Kama unaona mwanamke amekushinda zungumza kumuacha na ama kumrudisha kwao, ama kumruhusu aondoke, lakini siyo kumpiga. #BaloziWaWanawake #HK



14h

Comments