Majaribio ya dawa Hydroxychloroquine kuanza tena baada ya kusitishwa

Anti-malarial drugs
Majaribio yatagundua iwapo hydroxychloroquine inaweza kuzuwia maambukizi ya virusi vya corona

Majaribio ya dawa yenye utata ya malaria iliyomezwa na rais wa Marekani Donald Trump kujaribu kuzuwia kupatwa na virusi vya corona yanatarajiwa kufufuliwa tena.

Wasimamizi wa viwango nchini Uingereza wanasema hydroxychloroquine na dawa sawa na hiyo ya chloroquine inaweza kutolewa kwa wahudumu wa afya katika uchunguzi wa kimatibabu kupima dhana hiyo.

Shughuli ya kufanya majaribio ya hydroxychloroquine inayofahamika kwa lugha ya kitaalamu kama COPCOV ilikua imesitishwa kwa muda kutokana na tahadhari za madhara yake zilizoelezewa na watafiti wengine ambao hoja zao kwa sasa zimebainika kuwa hazina vigezo.

Majaribio yanaangalia jinsi ya kutibu Covid-19.
Ilibainisha kuwa dawa hiyo haikuwa na faida na inaongeza hatari ya kusababisha mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida na kifo.

Taarifa hiyo ilisababisha Shirika la afya duniani -WHO kusitisha majaribio yake ya kutibu virusi vya corona kwa hydroxychloroquine ambayo kwa kawaida hutibu malaria.

Hofu ilielezewa kuhusu data na halafu baadhi ya waandishi wa utafiti kuhusu dawa hiyo walisema kuwa hawana uhakika na maelezo yao wenyewe waliyoyaandika katika jarida la masuala ya tiba la Lancet huku kampuni ya huduma za afya ya Surgisphere ambayo ilihusika katika kazi ya utafiti huo wakikataa kuruhusu tathmini binafsi kuhusu dawa hiyo ifanyike.

Jarida la kitabibu la The New England lilipata waraka mwingine ambao ulikua na data kutoka kwa Surgisphere.

Dawa nafuu na inayopatikana kwa urahisi imekua ikitumika kuzuwia malaria kwa miaka.
coronavirus
Mtafiti mwenza Prof Martin Llewelyn, kutoka shule ya tiba za Brighton na Sussex Medical, anasema : "Ingawa viwango vya virusi vya corona ni vya chini kwa sasa nchini Uingereza , wahudumu wa afya bado wanaathiriwa na wimbi la pili la maambukizi linatarajiwa kwa kiwango kikubwa katika msimu wa majira ya baridi.

"Katika juhudi za kutafuta dawa inayoweza kuwalinda wahudumu muhimu wakati wa majira ya baridi, hydroxychloroquine inatumainiwa zaidi.''

Wakati huohuo, dawa za kupunguza makali ya virusi vya ukimwi lopinavir na ritonavir zimebainika kuwa hazina faida katika kuwazuwia wagonjwa wa corona kulazwa hospitalini.

Comments