RC Katavi akerwa na upinzani mkoani kwake ‘Kunizushia, Heti nimewataka waganga wa jadi kuwaroga’

Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera, amekerwa na wapinzani wake mkoani humo kwa kumzushia kauli ya kuagiza kurogwa kwa wananchi ili washiriki kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Kama ambavyo alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari hapa nchini.



Akiongea na Waandishi wa Habari mkoani humo, RC Homera amekanusha taarifa hiyo,  Ambapo amesema kauli yake aliwaomba watu wa Katavi kila mmoja kwa imani yake kuwaombea wapiga kura wajitokeze kwa wingi kuchagua viongozi bora siku ya uchaguzi wa Serikali za mtaa.



“Najua wanaofanya hivyo ni wenzetu wale wa upande wa pili, kwakuwa huku Katavi nimewashika pabaya nawanyoosha kama rula, Heti mimi nimewataka waganga kuwaroga watu, hawa wanaosema haya wamechanganyikiwa na hawajaanza leo wameshanizushia mambo mengi” Amesema RC Homera.

RC Homera amesema hii sio mara yake ya kwanza kuzushiwa na watu ambao yeye mwenyewe amedai wanatokana na masuala ya kisiasa.

“Nilipokuwa Tunduru walipiga picha darasa bovu, wakasema DC Tunduru amesema shida ya Darasa sio tatizo, shida na kipaumbele chake ni kukifuta chama fulani cha upinzani, kwahiyo hata haya ya kunizushia kuwa nimewataka waganga wa jadi kuwaroga watu siyashangai,” amesema RC Homera.

Comments