MUGABE KUZIKWA KATIKA MAKABURI YA MASHUJAA ZIMBABWE


Rais wa zamani wa Zimbabwe Robert Mugabe atazikwa kwenye makaburi yaliyoko kwenye kilele cha kilima, ambayo yamehifadhiwa makhsusi kwa watawala wa Zimbabwe.


Bado tarehe kamili ya maziko haijatangazwa na haijulikani ni lini mwili wa Robert Mugabe utarejeshwa nchini kutoka Singapore alikofariki wakati anapokea matibabu.

Mugabe aliyefariki akiwa na miaka 95 atazikwa katika makaburi ya mashujaa wa kitaifa kulikotengwa kwa raia wa zimbabwe waliyochangia pakubwa wakati wa vita dhidi ya utawala wa wazungu .

Comments