Waziri Lugola awaonya Polisi kuwabambikia kesi wananchi


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ametoa onyo kwa Polisi nchini ambao wanawafanya wananchi mtaji kwa kuwabambikiza kesi kisha kuwaomba pesa, kuacha tabia
hiyo mara moja na endapo wakibainika hatawavumilia, hatawaonea huruma hivyo sheria itafuata mkondo wake.

Amebainisha hayo katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata za Ilolangulu na Busabaga wilayani Mbogwe Mkoani Geita wakati amemuagiza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu kumsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbogwe (OC CID) Mkoani Geita, pamoja na Mkaguzi wa Jeshi hilo kwa kosa la kutuhumiwa kuomba na kupokea rushwa.

Kwa Upande wake Diwani wa Kata ya Ikobe, Wilayani humo, Costantine Kwezi, alimuomba Waziri kuwasaidia kukamilisha kituo cha polisi katika Kata yake na

Pia kuongeza idadi ya askari kituoni hapo, kwasababu kituo hicho kina askari mmoja ambaye anazidiwa na majukumu. Baadhi ya kina mama katika mkutano huo, nao walimuomba Waziri huyo kuwasaidia waume zao waliokamatwa kwa kosa la kusingiziwa kuwa ni majambazi kuachiwa huru, kutokana na kukosa hela ya kuhudumia familia na wao wameachwa bila kazi na watoto wadogo.

Comments