'Pango refu zaidi duniani la chumvi' lagunduliwa Israel

Mwanamke akiwa ndani ya pango Israel
Mwanamke akiwa ndani ya pango Israel
Watafiti nchini Israel wanasema wamegundua pango refu zaidi duniani la chumvi.

Njia na vichochoro vyenye urefu wa 10km ndani ya pango la Malham, linaloelekea katika bahari ya chumvi iliopakana na Jordan upande wa mashariki na Israel na ukingo wa magharibi upande wa magharibi vilivyowekwa kwenye ramani miaka miwili iliyopita.

Eneo hilo jangwani ni karibu na eneo ambako kwa mujibu wa biblia mkewe Lut aligeuzwa kuwa nguzo ya chumvi.

Wataalamu wanasema wanatarajia mvua kulirefusha pango hilo zaidi kadri muda unavyosogea.

Hili hufanyika wakati maji ya mvua yanapotiririka ndani ya upenoy wa pango hilo na kuyeyusha chumvi na kuunda njia zenye mlalo nusu zinazotiririka na kuelekea kwenye bahari ya chumvi.

Mawe ya chumvi
pango lenye chumvi
Sehemu ya pango hilo la Malham linalopitia Mlima wa Sodom, tayari lilikuwa limewekwa kwenye ramani katika miaka ya 80.

Miaka miwili iliyopita Yoav Negev kutoka kundi la watafiti wa mapango Israel aliamua kukamilisha uchunguzi huo na kuidhinisha kikosi cha watafiti na wataalamu wa masuala ya mapango.

Kwa wakati mmoja walipokuwa wakipumua ndani ya pango hilo, Boaz Langford kutoka chuo kikuu cha Hebrew mjini Jerusalem alisema wachunguzi hao walihisi kana kwamba chakula chao kimekosa kiungo.

"Basi tulikata chumvi kutoka mojawapo ya mawe na tukaitumia," alisema.

Chumvi ikiwa imening'inia kwenye pango
Malham imechukua rekodi ya miaka 13 inayoshikiliwa tangu mnamo2006 na pango lingine la chumvi lijulikanalo kama Cave of the Three Nudes, lenye urefu wa 6.85km katika kisiwa cha Qeshm nchini Iran, watafiti wameongeza


Comments