Uongozi wa Singida United wakanusha wachezaji kushidia ndizi


Uongozi wa klabu ya Singida United  inayoshirika ligi kuu Tanzania bara, umepingana na kauli za Makocha wao Popadic Dragan, na Dusan Momcilovic baada ya kueleza kuwa wanashindia ndizi mbivu na wamekuwa hawapewi fedha za nauli kuelekea mazoezini.

Siku mbili zilizopita Kocha Mkuu wa timu hiyo, Msebria Goran Popadic, alisema wamekuwa hawatimiziwi mahitaji yao muhimu ikiwemo nauli na mlo huku akieleza wamekuwa wakila mpaka ndizi kutuliza njaa kutoka na na ukata unaoikabili timu hiyo.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Singida United, Festos Sanga, ameibuka na kukanusha malalamiko ya Makocha hao kuwa si ya kweli, pia Sanga amekiri kuwa ni kweli Singida United inakabiliwa na ukata wa fedha lakini haijafikia hatua ya kushindwa kuwapa Makocha wake fedha za nauli na vyakula.

"Ni kweli timu ina ukata lakini si kweli yale yaliyozungumzwa na Makocha, hatuwezi kuwafanyia hivyo, wanapata mahitaji yote muhimu." alisema Sanga.

katika msimamo wa ligi kuu Singida United ipo nafasi ya 18 kwa kucheza michezo 27 na kujikusanyia alama 32 huku kushindwa michezo minane na kufungwa michezo minane.

Comments