Ujumbe aliotumiwa Samatta na timu yake ya Genk kabla ya mchezo, Balozi wa Uingereza Tanzania nae aliipongeza Stars

Taifa Stars imefanikiwa kufuzu Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kwa mara ya pili ikiwa ni maka 39 imepita tangu iingie kwenye michuano hiyo. Taifa Stars imefuzu kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Uganda, ambapo Matokeo mengine Lesotho imetoa sare ya 0-0 dhidi ya Cape Verde.


Goli la kwanza la stars lilifungwa na mshambuliaji Simon Msuva baada ya kupokea pasi kutoka kwa John Bocco. Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 1-0.

Dakika tano baada ya kipindi cha pili kuanza, Stars walipata penati baada ya mpira uliopigwa na nahodha Mbwana Samatta kutua kwenye mkono wa mlinzi wa Uganda Cranes Kirizistom Ntambi kwenye eneo la hatari.


Mkwaju wa penati hiyo ulisukumwa nyavuni na mlinzi Erasto Nyoni na kuiandikia Stars bao la pili.

Lakini pia timu ya mshambuliaji na nahodha wa taifa stars Mbwana Ally Samatta alitumiwa ujumbe huu na timu yake ya Genk kutoka nchini Ubelgiji.


Ushindi mnono kwa Stars ulihitimishwa katika dakika ya 57 mara baada ya beki Agrey Morris kufungwa kwa ustadi goli la kichwa akiunganisha krosi maridhawa iliyochongwa na John Bocco.
Ujumbe wa Twitter wa @Tanfootball: Hongera @taifastars_
Tff iliipongeza taifa stars

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Bi Sarah Cook naye ametuma saqlamu zake za hongera kwa ushindi huo uliosubiriwa kwa miaka 39.


Kufuzu kwa Stars kunakamilisha moja ya historia kubwa ya mafanikio ya mpira katika kanda ya Afrika Mashariki ambapo kwa mara ya kwanza mataifa manne ya ukanda huo yamefuzu kuelekea Misri.
Ujumbe wa Twitter wa @jmkikwete: Taifa Stars leo mmenipa raha. Ushindi mmoja, ndio mwanzo wa ushindi mwingine. Kila la kheri. #AFCON
Rais wa awamu ya nne Jakaya Mrisho Kikwete nae alitoa ujumbe wake

Uganda wao walitangulia kufuzu mwezi Novemba 2018, na michuano ya mwaka huu itakuwa ya saba kwa taifa hilo kushiriki.

Kenya ilikuwa ya pili kwa kufuzu katika ukanda huu kwa kufanya hivyo Disimba 2018., na wataenda Misri ikiwa ni mara yao ya sita kushiriki michuano hiyo.

Burundi wao walifuzu siku moja kabla ya Tanzania kwa kutoka sare na Gabon. Hii ni mara ya kwanza kwa taifa hilo kushiriki michuano ya AFCON.

Ujumbe wa Twitter wa @Tanfootball: Mataifa yaliyofuzu Afcon 2019
Kwa ujumla, michuano ya mwaka huu yatashirikisha mataifa 24, ikiwa ni ongezeko la timu 8 kutoka awali ambapo zilikuwa zikishiriki timu 16.

Comments