Salaam za rambirambi zaendelea kutolewa na mashabiki wa Clouds FM baada ya kifo cha Ephraim Kibonde

Ephraim Kibonde
Mtangazaji Mahiri wa Clouds FM Ephraim Kibonde aaga dunia
Salaam za rambirambi zimeendelea kutolewa, baada ya kutokea kifo cha Mfanyakazi na mtangazaji mahiri wa Clouds fm Ephraim Kibonde

Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dokta Thomas Rutachunzibwa ametoa taarifa kuhusu kifo cha Ephraim Kibonde kilichotokea alfajiri ya siku ya Alhamisi.

Hospitali ya Rufaa ya Kanda, Bugando ilipokea mwili wa marehemu Kibonde akitokea hospitali ya Uhuru jijini humo.


Kabla ya kufikishwa Mwanza Kibonde alipata huduma katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kagera.

Taarifa ya Mganga mkuu inasema umauti ulimkuta akiwa njiani kuelekea hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya kupata matibabu.

Taarifa ya Mganga mkuu inasema umauti ulimkuta akiwa njiani kuelekea hospitali ya rufaa ya Bugando kwa ajili ya kupata matibabu.

Ruka ujumbe wa Twitter wa @JMakamba

January Makamba

@JMakamba
 Nimesikitishwa sana na taarifa ya msiba wa rafiki yetu Ephraim Kibonde. Kipindi kigumu kwa familia ya Clouds - Joe, Sheba, Seba, Fauzia na wote. Kipindi kigumu zaidi kwa familia yake, hasa watoto wake. Tuwaombee uvumilivu na subira. Tumuombee marehemu apate pumziko la amani.

1,676
3:37 PM - Mar 7, 2019
Twitter Ads info and privacy
208 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @JMakamba
Ruka ujumbe wa Twitter wa @jmkikwete

Jakaya Kikwete

@jmkikwete
 Majonzi yangali nasi, nimepokea taarifa ya kifo cha Mtangazaji Ephrahim Kibonde wa @cloudsfm . Ni pigo kubwa kwetu sisi wapenzi wa kipindi cha Jahazi. Jahazi litaeleaje bila ya Nahodha Kibonde? Mwenyezi Mungu na aipe faraja familia yake, @cloudsfm na wasikilizaji wote wa Jahazi.

2,903
2:34 PM - Mar 7, 2019
Twitter Ads info and privacy
597 people are talking about this
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @jmkikwete
Ruka ujumbe wa Twitter wa @amufuruki
 Embedded video

Ali Mufuruki
@amufuruki
 The late Ephraim Kibonde who passed away early this morning worked for Infotech Group during the early days of his career. We will sorely miss his wisdom, friendship and kindness of spirit. May his soul R.I.P inshaallah @CloudsMediaLive @CEOrtTZ ⁦@tpsftz⁩

135
5:33 PM - Mar 7, 2019
19 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @amufuruki
Alianza kujisikia kuumwa tangu alipokua kwenye msiba wa Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji marehemu Ruge Mutahaba huko Bukoba.Kisha kupelekwa kwenye hospitali ya Bukoba kabla ya kuamua kumpeleka Mwanza.

Mkurugenzi wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga amesema mwili wa marehemu unatarajiwa kuwasili Dar es Salaam, leo Alhamisi usiku ukitokea jijini Mwanza.

Kibonde alikua mtangazaji mahiri wa kipindi cha JAHAZI cha Clouds fm, kipindi ambacho kimejizolea wasikilizaji wengi kutokana na namna yeye na watangazaji wenzie wanavyowasilisha maudhui mbalimbali ya kipindi hicho kinachoruka majira ya jioni kila siku.

Comments