MTANGAZAJI WA CLOUDS FM EPHRAIM KIBONDE KUZIKWA KESHO DAR


Mazishi ya aliyekuwa mtangazaji wa Kituo cha Redio Clouds Fm, Ephrahim Kibonde yatafanyika Jumamosi wiki hii.


Mwili wa Kibonde unatarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam leo Alhamisi Machi 7,2019 saa nne usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere na kuzikwa Jumamosi.

Joseph Kusaga, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group ametoa taarifa hiyo leo tarehe 7 Machi 2019 na kwamba, mwili wa Kibonde unatarajiwa kutua Dar es Salaam saa 4 usiku wa leo.

Amesema, baada ya kufika mwili huo utahifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo.

“Jana usiku niliongea na daktari Derrick aliyekuwa anamtibu Ephraim Kibonde akanihakikishia kuwa anaendelea vizuri lakini bahati mbaya wakati tunajiandaa kurudi Dar es Salaam hali ikabadilika na kusabaisha kifo chake.

“Taratibu za mazishi na maombolezo, zitafanyika kesho nyumbani kwake Mbezi na tunatarajia kuaga na kumpumzisha siku ya Jumamosi,” amesema Kusaga.

Comments