DC aagiza kuvunjwa kwa Mabaraza ya ardhi


Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, ameagiza kuvunjwa kwa mabaraza ya ardhi ya kata tatu ndani ya saa 24, kutokana na kulalamikiwa na wananchi kuhujumu haki za wananchi katika kumiliki ardhi.

Mabaraza hayo ni Machame Magharibi, Bomang’ombe na Bondeni pamoja kamati za ardhi vijiji vya Mkalama, Kawaya na Rundugai.

Amri hiyo ameitoa jana katika mkutano wa siku mbili wa kusikiliza kero, migogoro na malalamiko ya ardhi ya wananchi kata 17 za wilaya hiyo ambapo pia amesema mabaraza hayo yamekuwa chanzo kikuu cha migogoro ya ardhi.

"Hadi kufikia jana nilikuwa nimepokea malalamiko, migogoro na kero 266 ambazo ni kusogeza mipaka, urasimishaji makazi, fidia ya ardhi na zoezi la uwekaji alama za mipaka."

"Nakuagiza mwanasheria wa halmashauri (Henglibert Boniface) kwa kushauriana na mkurugenzi wako mtendaji ikifika kesho mniletee taarifa kuwa mmeshavunja mabaraza hayo," amesema.


Comments