Mazungumzo ya Trump na Kim yavunjika baada ya Korea Kaskazini kutaka kuondolewa vikwazo

Kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani Donald Trump
Kiongozi wa Korea Kaskazini na Rais wa Marekani Donald Trump
Mkutano kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un umemalizika bila kufikia makubaliano baada ya Marekani kukataa kutoa nafuu ya vikwazo kwa Korea Kaskazini, Rais wa Marekani ameeleza.

''Ilikuwa ni kuhusu vikwazo,'' Trump aliwaambia wanahabari.''Walitaka kuondolewa vikwazo na hatukuweza kufanya hivyo.''

Wawili hao walikua wanatarajiwa kutangaza maendeleo kuhusu mipango ya kukomesha matumizi ya silaha za Nuklia.

Trump amesema hakuna mipango yoyote iliyowekwa kwa ajili ya kufanyika kwa mkutano wa tatu.

Mipango ya awali ya Ikulu ya Marekani ilikua ni maandalizi ya sherehe za ''utiaji saini makubaliano'' pia chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya viongozi hao wawili, lakini matarajio yao yalizimwa kutokana na kuahirishwa kwa mkutano huo.

Sababu za kutofikiwa muafaka
Kwa Mujibu wa Trump, Kim alitoa ahadi muhimu- kuondoa vinu vya Yongbyon , vinavyotumika kufanya utafiti na uzalishaji Korea Kaskazini.Lakini kwa upande wake Kim alitaka vikwazo vyote viondolewe, kitu ambacho Marekani haikujiandaa kufanya hivyo.

Eneo la Yongbyon nchini Korea Kaskazini ni maarufu kwa upatikanaji wa kemikali ya plutonium lakini nchi hiyo ina takriban vinu viwili vinavyozalisha Uranium.

Pia rais Trump amesema kuwa Kim aliahidi uteketeza vinu vya Yongbyon pekee na si vinu vyote vya nuklia vya Korea Kaskazini.

Kim Jong un kukutana na Xi Jinping

Hii ni changamoto kwa Trump?

Mkutano wa kwanza kati ya viongozi hawa wawili, uliofanyika nchini Singapore mwezi Juni mwaka 2018, ulikosolewa kwa kutofikiwa kwa matarajio, hali iliyoleta hali ya kukisia kuwa Trump atashawishi kufanikisha hili katika mkutano wa Hanoi kufikia makubaliano ya kukomesha zana za nuklia.

Kushindikana kwa awamu hii ni changamoto kwa Trump, ambaye alizungumzia kuhusu umoja wao kuwa ni ishara ya mafanikio ya sera muhimu.

Mataifa mengine yanasema nini?
Taarifa ya ofisi ya rais nchini Korea Kusini imesikitishwa na kuvunjika kwa mkutano lakini amesema Marekani na Korea Kaskazini zilikua zimepiga ''hatua muhimu kuliko muda mwingine wowote waliokutana kabla ya mkutano wa Hanoi''

Kiongozi wa Korea Kusini, Moon Jae-in amefanya kazi kuhakikisha yanakuwepo mahusiano mazuri ya Korea zote mbili, na kusaidia kufanikisha mkutano wa nchini Singapore.

China nayo, mshirika mkuu wa Korea Kaskazini, imesema ina matumaini kuwa pande hizo mbili zitaendelea kuzungumza.

''Kutatua tatizo hili sio kazi yakufanyika siku moja,'' alieleza Waziri wa mambo ya nje, Lu Kang.
Mkutano wa pili wa Hanoi Vietnam umefanyika 28 February, 2019.
Bwana Kim na Trump wakiongozana walipokuwa na mazungumzo mjini Hanoi

Matokeo ya mkutano wao una ishara gani kwa mahusiano yao?

Walionekana kuwa na mahusiano mazuri katika mkutano wa Hanoi, kama ilivyokuwa nchini Singapore.Walipiga picha pamoja.

Akizungumza baada ya mazungumzo mjini Hanoi, Trump amesema uhusiano wao ''una nguvu sana''.

Comments