Gazeti The Citizen Tanzania lafungiwa kwa siku saba

The Citizen Tanzania lafungiwa kwa siku saba
The Citizen Tanzania lafungiwa kwa siku saba

Maoni mbalimbali yametolewa kutokana na hatua ya kusimamishwa kwa leseni ya uchapishaji na usambazaji wa gazeti la The Citizen kwa siku saba.

Serikali ya Tanzania imelifungia gazeti la hilo kwa madai ya kuchapisha taarifa ya upotoshaji kuhusu maoni ya watalaam waliozungumzia kuporomoka kwa shilingi.

Kufuatia kufungiwa huko kwa gazeti hilo la kila siku, kumeibua maoni tofauti miongoni mwa wananchi, wachambuzi na wadau mbalimbali wa habari.

Kufuatia kufungiwa huko kwa gazeti hilo la kila siku, kumeibua maoni tofauti miongoni mwa wananchi, wachambuzi na wadau mbalimbali wa habari.

 @The_EastAfrican

The EastAfrican

@The_EastAfrican
 TANZANIA has banned the publication of The Citizen newspaper for seven days, effective today, after it published a story on depreciation of the shilling against the dollar on February 23.

347
6:15 PM - Feb 27, 2019
427 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @The_EastAfrican
Ruka ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe
View image on TwitterView image on TwitterView image on TwitterView image on Twitter

Zitto Kabwe Ruyagwa

@zittokabwe
 After suspension of Tanzanian leading daily paper, The Citizen, Foreign exchange shops ( Bureau de Change ) are being closed. Why this panic ?

360
12:05 PM - Feb 28, 2019
126 people are talking about this
Twitter Ads info and privacy
Mwisho wa ujumbe wa Twitter wa @zittokabwe
Mamlaka zimeshutumu gazeti hili la kila siku kukiuka maadili katika uchambuzi wake wa makala mbalimbali.Lakini makundi ya upinzani na asasi za kiraia miezi ya hivi karibuni walikosoa utawala wa Rais Magufuli kwa kukandamiza uhuru wa habari nchini Tanzania, madai ambayo yalikanushwa.

Msajili wa magazeti nchini Tanzania, Patrick Kipangula amethibitisha hilo kutokana na taarifa kuhusu kuporomoka kwa shilingi iliyochapishwa juma lililopita.Mhariri wa gazeti hilo amesema wameshtushwa na uamuzi wa serikali lakini hakuwa tayari kueleza zaidi.

Magufuli ayaonya magazeti Tanzania

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita karibu magazeti 7, likiwemo gazeti la Mseto, Mwanahalisi, Mawio, Tanzania Daima na Raia Mwema, na sasa the citizen yamefungiwa kwa nyakati tofauti kwa makosa mbalimbali.

Wauza magazeti wameguswa na hatua hii ya serikali baadhi wanaona kuwa vipato vyao viko hatarini." Hata kama Napata shilingi 1,500 mimi inanisaidia, kwa sababu mimi kazi yangu ni kuuza magazeti,unavyofungia gazeti moja, mawili ama matatu, unakiathiri kipato changu na maisha yangu.'' alieleza Ramadhan Ramdhan.

Comments