Baada ya kipigo kutoka Simba, kocha wa Azam kaulizwa hofu ya kufukuzwa


Baada ya game ya Azam FC dhidi ya Simba SC kumalizika kwa Simba kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli yakifungwa na Meddie Kagere dakika ya 4 na 77 na John Bocco akafunga goli jingine dakika ya 38 wakati Frank Domayo dakika ya 81 akaifungia Azam FC goli la kufutia machozi na kuifanya Simba kuvuna point tatu.

Kocha mkuu wa Azam FC Hans van Pluijm ameongea sababu za kikosi chake kuruhusu kufungwa dhidi ya Simba kuwa ni kutokana na wachezaji wake kutojiamini licha ya kufanikiwa kumiliki mpira kwa kiasi fulani, kama wangejiamini anaamini mambo yangeweza kuwa tofauti, Hans alipoulizwa ishu za hofu ya kupoteza kibarua chake alisema kocha ana ajiriwa ili afukuzwe.

“Tumetawala mchezo kwenye mechi ya leo lakini hatukupata ushindi kwa sababu wachezaji wangu hawajiamini, kuhusu hofu ya kufukuzwa? hilo ni aina ya swali ambalo unatakiwa kuwauliza uongozi maana makocha wanaajiriwa ili wafukuzwe, mimi najaribu kufanya vizuri kwa uwezo wangu na najaribu kuhakikisha wachezaji wangu wanafanya vizuri pia”>>>Hans van Pluijm

Comments