Ukristo na Uislamu: Uhusiano wa dini ya Kiislamu na Yesu na Maria

Kidole kikionyesha kwenye Koran ambapo Yesu ametajwa
Kidole kikionyesha kwenye Koran ambapo Yesu ametajwa

Katika mataifa yenye Wakristo wengi, kwa sasa kila kitu ni Krismasi. Ni nadra kufikiria kwamba kuna maeneo ambapo sikukuu hii haitambuliwi kama kidogo.
Ni siku tu ya kawaida.
Miongoni mwa mataifa ambayo Krismasi haitambuliwi kama sikukuu rasmi ni mataifa ya Kiislamu. Mfano nchini Uturuki, 25 Desemba huwa siku tu ya kawaida kwenye kalenda.
Sababu kuu ni kwamba huwa ni sikukuu ya kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu, nabii mkuu katika dini za Kikristo.

Shoppers walk among Christmas lights in Berlin
Mapambo ya Krismasi jijini Berlin

Sikukuu hii haipo kwenye kalenda za Kiyahudi, Kihindi au Kikristo.
Miongoni mwa Waislamu, ukuu wa sikukuu hii unakaribiana tu pengine na sikukuu za Eid. Ndio wakati Waislamu hukutana kama familia, na kujumuika pamoja na marafiki na hata kufufua urafiki na watu waliokosana nao. Aidha, huwasaidia wasiojiweza.
Kufahamu tofauti hizi ni muhimu sana, usije kumtakia Mwislamu Heri ya Sikukuu ya Krismasi.
Lakini si kwamba Yesu hatambuliwi kwenye dini ya Kiislamu.

Jesus, unamaanisha Isa?
Hili huwashangaza wengi wasiolifahamu.
Waislamu huwa hawasherehekei siku ya kuzaliwa kwa Yesu, lakini humuenzi.
Waislamu huonyesha heshima kuu kwa nabuu huyu wa Kiksrito na humtambua kama sehemu muhimu ya imani yao.
Mchoro wa Bikira Maria uliochorwa na Mwislamu, kama anavyoelezwa kwenye KoranHaki miliki ya pichaHAJULIKANI
Image caption
Mchoro wa Bikira Maria uliochorwa na Mwislamu, kama anavyoelezwa kwenye Koran
Koran humchukulia Yesu kama mmoja wa manabii wa kuheshimiwa sana waliomtanglia Mtume Muhammad (S.A.W.- Sallā Allāhu ʿalayhi Wa-sallam).
Yesu kwa Kiarabu hufahamika kama Isa, na ametajwa mara nyingi sana kwenye Koran, hutajwa sana hata kumshinda Muhammad kwenye Koran.
Isitoshe, yupo mwanamke mmoja pekee aliyetajwa kwa jina kwenye kitau hicho kitukufu cha dini ya Kiislamu.
Mchoro wa Bikira Maria uliochorwa na Mwislamu, kama anavyoelezwa kwenye Koran
HAJULIKANI
Image caption
Mchoro wa Bikira Maria uliochorwa na Mwislamu, kama anavyoelezwa kwenye Koran

Mary au Maryam
Mwanamke huyo ni Bikira Maria, ambaye kwa Kiarabu hujulikana kama Maryam.
Ameangazia kwenye aya zima kwenye Koran, ambapo inasimuliwa kuhusu alivyomzaa mtoto akiwa bikira.
Tofauti kati ya Eid ul-Fitr na Eid ul-Adha
Lakini hadithi ya kuzaliwa kwa Yesu kwenye Uislamu haijamtaja Yusufu popote, wala wale manajimu kutoka Mashariki, wala kulazwa kwenye hori ya kuwalishia ng'ombe.
Maria anajifungua akiwa peke yake jangwani, akiwa amejikinga chini ya mnazi uliokauka.
Mwujiza unatokea na tende zilizoiva zinaanguka kutoka kwenye mnazi huo na kuwa chakula chake.

Aidha, mto wenye maji safi unachipuka kutoka miguuni mwake na kumpa maji.
Sleep of the Child Jesus, by Italian artist Giovanni Battista SalviHaki miliki ya pichaGETTY
Sleep of the Child Jesus, by Italian artist Giovanni Battista Salvi
Hadithi ya Maria na kujifungua kwake akiwa bikira inafahamika sana
Mwanamke ambaye hajaolewa kujifungua ni kisa ambacho kinazua maswali mengi sana kuhusu maadili yake.
Lakini mtoto huyo - Yesu - anapozaliwa, anaanza kuzungumza kama nabii wa Mungu.
Mwujiza huo unamuondolea ndoa mamake.
Ni hadithi ya ushindi dhidi ya ubaguzi na hukumu.
Nabii wa nyoyo za watu
Waislamu wanapomrejelea Yesu, huwa wanatakiwa kutamka S.A.W. (Sallā Allāhu ʿalayhi Wa-sallam), kwa maana ya Amani Iwe Naye, sawa na wafanyavyo kwa Mtume Muhammad.
Waislamu kuwa wengi kuliko Wakristo duniani
Na je, nani anayetarajiwa kurejea duniani siku ya Kiyama na kurejesha haki duniani, kwa mujibu wa dini ya Kiislamu?
Ni Yesu, huo ukiwa ujio wake wa pili, na kutukuzwa kwake katika vitabu vya Kiislamu sio tu katika Koran.
Mwanafalsafa wa Kisufi Al-Ghazali anamweleza kama "nabii wa nyoyo".
Ibn Arabi anaandika kumhusu yeye kuwa "muhuri wa watakatifu".
Benedict: Nilikuwa ninaabudu shetani
Kote katika ulimwengu wa Kiislamu, kuna wavulana wanaopewa jina Isa (Yesu) na wasichana wanaoitwa Maryam, kutokana na Maria au Mary.
Unaweza kutafakari mtu kutoka familia ya Kikristo akimbatiza mtoto wake jina Muhammad?
Dini ya Kiislamu inamfahamu vyema Yesu, kwa sababu kufikia wakati wa kuwa dini katika karne ya 7, dini ya Kikristo ilikuwa tayari imekita mizizi Mashariki ya Kati.

The Basilica of San Petronio is the main church of Bologna

Watu watano walikamatwa wakituhumiwa kupanga kushambulia katisa la San Petronio nchini Italia
Muhammad hajatajwa popote katika Biblia.
Ingawa dini ya Kiislamu humuenzi Yesu, katika karne za baadaye, ni kweli kwamba dini ya Kikristo haikuwa inarejesha fadhila hizo.

Nabii huyo mkuu wa Kiislamu anaonyeshwa jahannamu, akiwa anateswa na mashetani, katika mchoro mkubwa wa karne ya 15 unaopatikana katika kanisa kuu la San Petronio katika jiji la Bologna nchini Italia.
Kuna michoro mingi na kazi za sanaa zinazomuonyesha vibaya Mtume Muhammad.
Mduara wa tisa wa jahannamu

Mchoraji Mwitaliano Giovani da Modena aliongozwa na simulizi za mshairi maarufu Dante Alighieri ambaye hufahamika tu kama Dante, ambaye alimuweka Muhammad kwenye mduara wa tisa wa jahannamu katika kitabu chake cha shairi ndefu la Divine Comedy.
Kitabu hicho kiliwahamasisha wasanii na wachoraji wengi wa Ulaya hadi karne ya 1800 kwenye michoro yao ya Mtume Muhammad inaomuonyesha akiadhibiwa kwenye moto wa jahannamu.
Imam Sami Salem (L) and Imam Mohammed ben Mohammed (R) wakiwa Santa Maria church in Rome
Wahubiri wa Kiislamu wameshiriki ibada katika makanisa ya Katoliki nchini Italia kushutumu mashambulio ya kijihadi

Miongoni mwa michoro hiyo ni ule wa William Blake, msanii maarufu England kwa michoro na mashairi yake.
Katika kanisa moja la Ubelgiji, eneo la ibada lililopambwa karne ya 17 linamuonyesha mtume huyo wa dini ya Kiislamu akiwa amelazwa chini na kukanyagwa na malaika kwa miguu yao.
Msimamo wa kanisa na dini ya Kikristo ulibadilika baadaye.
Lakini enzi za sasa zina chuki zake na uhasama.

Ushirikiano wa kidini

Mwaka 2002, wanamgambo wa Kiislamu walituhumiwa kutaka kulipua mchoro huo wa kanisa la Bologna.
Tangu wakati huo, kumetokea mashambulio mengi yaliyosababisha vifo vya watu, yaliyotekelezwa kwa jina la dini ya Kiislamu katika mataifa mengi ya Ulaya na Kiislamu. Mashambulio hayo yameendeleza kuzidisha ufa kati ya dini hizo mbili.
Kufahamu kuhusu Yesu na Uislamu pamoja na kufahamu umuhimu wake katika dini hiyo kwa sasa kunaweza kuwasaidia Waislamu an Wakristo kuridhiana.
Pengine, kuangazia mambo ya pamoja na badala ya tofauti kunaweza kusaidia kumaliza uhasama uliopo.

Comments