Obamacare: Mahakama imesema kuwa bima hiyo inakiuka sheria

Watu wakijisajili kwa bima hiyo kaitika miji ya Miami, Florida. Novemba mosi mwaka 2017
Jaji wa jimbo la Texas nchini Marekani ameamuru kuwa badhi ya vipengele vya sheria katika bima ya afya maarufu kama Obamacare, vinakiuka katiba.
Majimbo 26 yalihoji kuwa mwongozo wa sheria za bima hiyo umepitwa na wakati baada ya mswada wa ushuru kuidhinishwa kuwa sheria mwaka jana.
Sheria hiyo mpya iliondoa faini dhibi watu ambao hawajajisajili kwa mpango huo wa afya.
Rais wa Marekani Donald Trump amesema uamuzi huo ni habari njema kwa Wamarekani.

Uamuzi huo unakuja siku moja kabla ya kumalizika kwa muda wa mwisho wa kujisajili kwa bima hiyo mwakani kukamilika.
Sheria inayoongoza bima hiyo hata hivyo itaendelea kutumika hadi uamuzi huo utakapo amuliwa na mahakama ya juu zaidi ya Marekani.
Baada ya Uamuzi huo kutolewa rais Trump alisema aliandika maneno haya katika mtandao wake wa Twitter...

Ujumbe wa Twitter wa @realDonaldTrump: Wow, but not surprisingly, ObamaCare was just ruled UNCONSTITUTIONAL by a highly respected judge in Texas. Great news for America!

Pia alitoa wito kwa kwa kiongozi wa chache katika bunge la seneti Chuck Schumer na spika wa bunge Nancy Pelosi "Kupitisha sheria madhubuti ambayo itasimamia huduma bora ya afya".
Wakati wa kampeini yake ya Urais Trump aliahidi kufutilia mbali mpango huo wa Afya uliyobuniwa na mtangulizi Obama mwaka 2010, ili kuwapatia raia wa nchi hiyo bima ya afya ya gharama nafuu.
Licha ya chama cha Republican kuwa na wabunge wengi katika mabunge yote mawili imeshindwa kufutilia mbali Obamacare.

Hata hivyo mwaka 2017 bunge lilifanyia marekebisho bima hiyo ili kuwaruhusu wafanyibiashara wadogo na watu binafsi kuungana na kuanzisha miungano na kufadhili usimamizi wa bima mbadala kulingana na sheria ya majimbo yote ya Marekani.
Umuzi huo una sema nini?
Wanasheria wakuu wa republican kutoka majimbo ya Texas na Wisconsin waliongoza kesi iliyowasilishwa dhidi ya bima hiyo.
Jaji Reed O'Connor alisema kuwa mswada wa ushuru wa dola trilioni 1.5 ambao ulipitishwa na bunge mwaka 2017 ulifutilia mbali faini dhidi ya mtu yeyote atakayekosa kulipia bima hiyo.
Aliamuru kuwa sharti la lazima kwa mtu binafsi kuchukua bima hiyo ni kinyume cha sheria.
Jaji O'Connorpia alisema uamuzi wake umezingatia zaidi dhamira ya bunge ya mwaka 2010 na 2017.
watu waandamana kuhusiana na suala hilo
Sheria ya bima ya afya imekuwa suala tata nchini Marekani kwa muda mrefu

Hatua hiyo imepokelewaje?
Spika wa bunge Nancy Bi Pelosi ameutaja uamuzi huo kama wa "ukatili" na wa "kusikitisha" na kuongeza kuwa utabatilishwa.
Ameongeza kuwa uamuzi huo unaonesha kadhia ya "kutojali ya warepublican' akisema lengo lao ni kuwanyima watu kupata bima ya matibabu ya gharama nafuu ".
Kwa upande wake bwana kiongozi wa wachache katika bunge la seneti Chuck Schumer, amesema uamuzi huo "unaegemea upande mmoja na kwamba unazingatia masuala yasiyokuwa na msingi".
Nini Kitakachofuata?
Umuzi huo bila shaka utapingwa katika mahakama ya juu zaidi ya Marekani.
Msemaji wa wa ikulu ya Marekani Sarah Sanders amesema sheria hiyo tata itaendelea kutumika ikisubiri hadi pale mzozo wa kisheria kuihusu itakapotatuliwa
Huku hayo yakijiri,White House imetoa wito kwa bunge kubadilisha mpango wa Obamacare na bima nyingine ya afya ambayo itawahudumia watu bila vikwazo.
Baadhi ya majimbo ya Marekani yanahoji kuwa kufutilia mbali mpango huo kutawaathiri mamilioni ya watu nchini humo.
Kiongozi wa Demokratic katika bunge la seneti Chuck Schumer amesema: "Uamuzi huo mbaya ukidumishwa katika mahakama ya juu itakuwa ni pigo kwa mamilioni ya familia za Marekanis."

Comments