Waziri ashtakiwa akiwataka waislam kuchukuwa likizo kipindi cha Ramadhan

Waziri Ashtumiwa Akitaka Waislam Wachukue Likizo Kipindi cha Ramadhani
Waziri wa uhamiaji wa Denmark ameshtumiwa vikali kutokana na pendekezo alilolitoa la kuwataka Waislam wachukue mapumziko wakati wa mwezi wa Ramadhani kwa usalama wa jamii nchini humo.

Inger Stojberg, ambaye amekuwa akifahamika kwa kutekeleza sera kali za uhamiaji, amesema kufunga saa za kazi siku nzima kunaleta changamoto katika kazi.

Amedai kuwa kunaweza kusababisha hatari hasa kwa waendesha mabasi ya abiria na wafanyakazi wa hospitalini kufanya kazi muda mrefu bila kula.

”Natoa wito kwa Waislamu kuchukua likizo wakati wa mwezi wa Ramadhani kuepuka madhara kwa jamii nzima ya Denmark” amesema Waziri Inger 

Comments