Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 21.05.2018

Meneja wa Chelsea Antonio Conte
Meneja wa Chelsea Antonio Conte

Manchester City wanampango wa kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard,27, kwa mkataba wa £100m baada ya meneja Pep Guardiola kumuweka mchezaji huyo kuwa kiungo muhimu anayemlenga wakati wa uhamisho.(Star)
Klabu ya Utaliano ya AC Milan imempatia kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini,30, mkataba wa miaka mitatu huku kiungo huyo raia wa Ubelgiji kuwa huru kwa uhamisho wa bure katika majira ya joto. (Times - subscription required)
Conte: Nitamsalimia Mourinho kwa mkono
Beki wa Tottenham,Toby Alderweireld, 29, ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuuzwa na klabu ya United wakati wa uhamisho wa majira ya joto. (Mirror)
West Ham inaamini kumteuwa Manuel Pellegrini kama meneja wao mpya wiki hii- ambayo itaipatia nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati Yaya Toure, 35, aliyeiaga Manchester City. (Telegraph)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anatarajiwa kuiaga Chelsea kwa saa 48 zijazo - huku meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo. (Express)
Jack Wilshere

Jack Wilshere
Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26 yuko tayari kutia saini mkataba wa miaka mitatu aliyopewa na Arsenal , licha ya kupata mapendekezo bora kutoka Everton na Wolves. (Mirror)
Manchester United wavuna zaidi ya Manchester City EPL
Manchester United imekubaliana katika hatua za kwanza na kiungo wa kati kutoka Brazil Talisca, 24 ambaye amekuwa kwenye mkopo na Besiktas kutoka Benfica. (Star)
Uteuzi wa Kocha wa zamani wa Paris St-Germain Unai Emery umewashangaza wengi baada ya kuteuliwa katika dakika za mwisho kuwa meneja mpya wa Arsenal. (Mail)

Thibaut Courtois
Mlinda mlango kutoka Ubelgiji Thibaut Courtois

Mlinda lango kutoka Ubelgiji Thibaut Courtois, 26 ametishia kuihama Chelsea iwapo klabu hiyo haitatumia pesa zake kama klabu za ''Manchester United na City'' msimu huu wa joto. (Sun)
Mazungumzo ya Napoli na meneja wao Maurizio Sarri yametibuka kutokana na mataminio ya meneja huyo kutaka kuihamia Chelsea. (Mirror)
Mhispania Santi Cazorla ,33, amepewa nafasi ya kujiunga na klabu yake ya zamani ya Villarreal huku mkataba wake na Arsenal ukitarajiwa kukamilika. (Evening Standard).

Kiungo wa kati wa Ac Milan Suso
Kiungo wa kati wa Ac Milan Suso

Kiungo wa kati wa Ac Milan Suso, 24,anatarajiwa kurudi Liverpool lakini si kwa mara moja kwa siku zijazo. (Liverpool Echo)
Beki Partick Thistle Niall Keown, 23, anatarajiwa kubadili majukumu yake kutoka Republic hadi Kaskazini mwa Ireland - na meneja Michael O'Neill anataka kumsajili kiungo wa kati wa Klabu ya QPR Sean Goss, 22, kwa mkopo. (Daily Record)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefuta akaunti yake ya Instagram kutokana na matusi ambayo aliyoyapata baada ya mashetani hao wekundu kushindwa kwenye fainali ya kuwania kombe la FA dhidi ya Chelsea. (Sun)

Comments